na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, wa kwanza kufufuliwa kutoka kwa wafu, na ambaye ni mtawala wa wafalme wa dunia. Yeye anatupenda na ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu yake;

akatufanya sisi kuwa wafalme na makuhani, tum tumikie Mungu Baba yake. Utukufu na uwezo ni wake milele na milele! Amina.

Tazama! Anakuja katika mawingu! Na kila jicho litamwona. Hata na wale waliomchoma mkuki na makabila yote ulimwenguni wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.

Read full chapter