Add parallel Print Page Options

Nakuandikia wewe Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki:

Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba, na kutoka kwa Kristo Yesu[a] Mwokozi wetu iwe nanyi.

Kazi ya Tito Krete

Nilikuacha kule Krete ili uweze kuyakamilisha yale yaliyokuwa yamebaki kufanyiwa kazi. Kisha nakuagiza uteue wazee na kuwaweka kuwa viongozi katika kila mji. Anayeweza kuteuliwa ni yule ambaye halaumiwi kwa matendo yoyote mabaya, na aliye mwaminifu kwa mkewe,[b] na anao watoto wanaoamini Mungu[c] na ambao sio wakaidi.

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:4 Kristo Yesu Au “Mfalme Yesu”. Neno “Kristo” ni tafsiri ya Kiyunani ya neno la Kiebrania “Masihi”, ambao ni wadhifa wa kifalme. Tazama Mk 15:32: Lk 23:2. Tazama pia Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno.
  2. 1:6 mwaminifu kwa mkewe Kwa maana ya kawaida, “mtu mwenye mke mmoja”, yenye maana pia ameoa mara mmoja tu.
  3. 1:6 wanaoamini Mungu Neno hli laweza kuwa na maana ya “waaminifu” au “waaminio”. Hapa, maana zote zaweza kujumuishwa. Linganisha kifungu hiki na 1 Tim 3:4.