Add parallel Print Page Options

Hivyo, hivi ndivyo mnapaswa kuomba:

‘Baba yetu uliye mbinguni,
    Jina lako lipewe utukufu.
10 Ufalme wako uje.
Mapenzi yako yafanyike hapa dunia,
    kama yanavyofanyika huko mbinguni.
11 Utupe leo chakula tunachohitaji.
12 Utusamehe dhambi zetu,
    kama tunavyowasamehe wale wanaotukosea.
13 Usiruhusu tukajaribiwa,
    lakini utuokoe na Yule Mwovu.’[a]

14 Mkiwasemehe wengine makosa waliyowatendea, Baba yenu wa mbinguni naye atawasamehe makosa yenu pia. 15 Lakini msipowasamehe wengine, Baba Yenu wa mbinguni hatawasamehe ninyi.

Read full chapter

Footnotes

  1. 6:13 Nakala zingine za Kiyunani zimeongeza: “Kwa kuwa ufalme na nguvu na utukufu ni vyako milele na milele. Amina.”