Yesu Na Beelzebuli

22 Kisha wakamletea kipofu mmoja ambaye pia alikuwa bubu na amepagawa na pepo. Yesu akamponya akaweza kusema na kuona. 23 Watu wote wakashangaa wakaulizana, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?” 24 Lakini Mafarisayo waliposikia haya wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mfalme wa pepo wote.”

25 Yesu alifahamu mawazo yao, akawaambia, “Utawala wo wote ambao umegawanyika wenyewe kwa wenyewe utaanguka. Hali kadhalika mji wo wote au jamaa ye yote iliyogawanyika yenyewe kwa yenyewe haitadumu. 26 Na kama shetani anamfukuza shetani, atakuwa amega wanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utaendeleaje? 27 Na kama mimi hutoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, watu wenu je, wao hutoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao ndio watakaowaamulia. 28 Lakini kama ninatoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia. 29 Au inawezekanaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang’anya mali yake yote pasipo kwanza kumfunga yule mwenye nguvu? Akisha mfunga ndipo hakika anaweza kupora mali yake.

30 “Mtu asiyekuwa pamoja nami ananipinga; na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, anatawanya.

Read full chapter