Add parallel Print Page Options

Kisha Shetani alimwongoza Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerusalemu na akamweka juu ya mnara wa Hekalu. Akamwambia Yesu, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe mpaka chini! Kwani Maandiko yanasema,

‘Mungu atawaamuru malaika zake wakusaidie,
na mikono yao itakupokea,
    ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’”(A)

Yesu akamjibu, “Pia, Maandiko yanasema, ‘usimjaribu Bwana Mungu wako.’”(B)

Read full chapter