Add parallel Print Page Options

24 Mwana wa Adamu atakiendea kifo chake kama Maandiko yanavyosema. Lakini ole wake mtu yule anayemsaliti Mwana wa Adamu ili auawe. Ni bora mtu huyo asingezaliwa.”

25 Ndipo Yuda, ambaye ndiye angemsaliti, akamwambia Yesu, “Mwalimu, hakika si mimi unayemzungumzia, ama ndiye?”

Yesu akamjibu, “hicho ndicho unachosema.”

Chakula cha Bwana

(Mk 14:22-26; Lk 22:15-20; 1 Kor 11:23-25)

26 Walipokuwa wakila, Yesu alichukua baadhi ya mikate na akamshukuru Mungu. Alimega baadhi ya vipande, akawapa wafuasi wake na akasema, “Chukueni mkate huu na mle. Ni mwili wangu.”

Read full chapter