Add parallel Print Page Options

Akiwa njiani kuelekea Yerusalemu, watu wengi walitandaza mavazi yao barabarani kwa ajili Yake. Wengine walikata matawi ya miti na kuyatandaza barabarani ili kumkaribisha. Wengine walimtangulia Yesu, na wengine walikuwa nyuma yake. Wote walipaza sauti wakisema:

“Msifuni[a] Mwana wa Daudi!
‘Karibu! Mungu ambariki yeye
    ajaye katika jina la Bwana!’(A)
Msifuni Mungu wa mbinguni!”

10 Kisha Yesu aliingia Yerusalemu. Watu wote mjini wakataharuki. Wakauliza, “Mtu huyu ni nani?”

Read full chapter

Footnotes

  1. 21:9 Msifuni Yaani, “Hosanna”, ambalo ni neno la Kiebrania lililotumika kumwomba msaada Mungu. Hapa, labda ilikuwa ni kelele ya shangwe iliyotumika kumsifu Mungu au Masihi wake. Pia mwishoni mwa mstari huu na pia katika mstari wa 15.