Font Size
Mathayo 16:16-18
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 16:16-18
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
16 Simoni Petro akajibu, “Wewe ni Masihi, Mwana wa Mungu aliye hai.”
17 Yesu akajibu, “Umebarikiwa, Simoni mwana wa Yona. Hakuna aliyekufundisha hilo ila Baba yangu wa mbinguni ndiye amekuonesha mimi ni nani. 18 Hivyo ninakwambia, Wewe ni Petro. Na nitalijenga kanisa langu kwenye mwamba[a] huu. Nguvu ya mauti[b] haitaweza kulishinda kanisa langu.
Read full chapterFootnotes
- 16:18 Petro … mwamba “Petro”, ni jina la Kiyunani (Kigiriki) ambalo kwa Kiaramu ni “Kefa” likimaanisha “mwamba”. Katika Maandiko (Isa 51:1,2), pamoja na desturi za Kiyahudi, Ibrahimu alilinganishwa na mwamba ambao Mungu angeutumia “kujengea” watu wake. Hivyo Yesu anaweza kulinganisha kuwa Yesu ni kama Ibrahimu. Mungu aliwapa majina mapya Ibrahimu na Sara na aliwaheshimu kama mifano ya imani kwa wazaliwa wao. Katika namna hiyo hiyo, Yesu alimpa jina jingine Petro (tazama Mk 3:16) na akamheshimu hapa kwa ujasiri wake wa imani.
- 16:18 Nguvu ya mauti Kwa maana ya kawaida, “malango ya Kuzimu”.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International