Font Size
                  
                
              
            
Mathayo 11:23-25
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 11:23-25
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
23 Nawe Kapernaumu, utakwezwa mpaka mbinguni? Hapana! Utatupwa chini mpaka Kuzimu. Nimetenda miujiza mingi ndani yako. Iwapo miujiza hii ingetokea Sodoma,[a] watu huko wangeacha kutenda dhambi na ungekuwa bado ni mji hata leo. 24 Lakini ninakuambia, itakuwa vibaya kwako siku ya hukumu kuliko Sodoma.”
Yesu Awapa Pumziko Watu Wake
(Lk 10:21-22)
25 Kisha Yesu akasema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbinguni na duniani. Ninashukuru kwa sababu umeyaficha mambo haya kwa wale wanaofikiri kuwa ni wenye hekima na werevu sana. Lakini umeyaonesha haya kwa watu walio kama watoto wadogo.[b]
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU) 
    © 2017 Bible League International