Font Size
Mathayo 11:21-23
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 11:21-23
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
21 Yesu alisema, “Itakuwa vibaya kwako Korazini! Itakuwa vibaya kwako Bethsaida![a] Ikiwa miujiza hii hii ingetokea Tiro na Sidoni,[b] watu huko wangeshabadili maisha yao kitambo. Wangekwishavaa magunia na kujimwagia majivu kuonesha kuwa wanasikitikia dhambi zao. 22 Lakini ninawaambia, siku ya hukumu itakuwa vibaya zaidi kwako kuliko Tiro na Sidoni.
23 Nawe Kapernaumu, utakwezwa mpaka mbinguni? Hapana! Utatupwa chini mpaka Kuzimu. Nimetenda miujiza mingi ndani yako. Iwapo miujiza hii ingetokea Sodoma,[c] watu huko wangeacha kutenda dhambi na ungekuwa bado ni mji hata leo.
Read full chapterFootnotes
- 11:21 Korazini, Bethsaida Miji ya Kiyahudi iliyokuwa kando kando mwa Ziwa Galilaya ambapo Yesu alifanya miujiza mingi kudhihirisha mamlaka yake yanayotoka kwa Mungu. Pamoja na hili, watu walikataa kubadili maisha waliyoishi yasiyokuwa na Mungu.
- 11:21 Tiro na Sidoni Miji iliyojaa ibada ya sanamu ambayo ilijulikana sana kwa uovu uliokuwemo humo.
- 11:23 Sodoma Mji ambao Mungu aliuangamiza, pamoja na Jiji la Gomora, kwa sababu watu walioishi walikuwa waovu sana. Tazama Mwa 19.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International