25 Nao wali pokwisha kutoa ushuhuda na kufundisha neno la Bwana, walirudi Yerusalemu; na walipokuwa wakisafiri walihubiri Habari Njema katika vijiji vingi vya Samaria.

Filipo Ambatiza Afisa Wa Ethiopia

26 Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara itokayo Yerusalemu kuelekea Gaza.” Hii ilikuwa barabara iendayo jangwani. 27 Filipo akaondoka akaenda. Wakati huo Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa waziri wa fedha wa Kandake, Malkia wa Ethiopia, alikuwa anarudi nyumbani baada ya kumwabudu Mungu huko Yerusalemu.

Read full chapter