31 Walipokwisha kusali, nyumba waliyokuwa wamekutania ikatikisika na wote wakaja zwa na Roho Mtakatifu, wakahubiri neno la Mungu kwa ujasiri. 32 Waamini wote walikuwa na nia moja na moyo mmoja, wala hakuna aliyeona mali aliyokuwa nayo kuwa yake, bali walishirikiana vitu vyote kwa pamoja. 33 Na kwa uwezo mkubwa mitume wakashuhudia kwa ujasiri habari za kufufuka kwa Bwana Yesu. Mungu akawapa wote neema kuu.

Read full chapter