24 Waamini wote waliposikia maneno yao walimwomba Mungu kwa pamoja wakasema, “Wewe Bwana Mtukufu, uliyeumba mbingu na nchi na bahari na kila kiumbe kilichopo, 25 wewe ulitamka kwa njia ya Roho wako mtakatifu kupitia kwa baba yetu Daudi mtumishi wako, aliposema, ‘Mbona mataifa wanaghadhabika, na watu wanawaza mambo yasiyo na maana? 26 Wafalme wa dunia wamejiandaa na watawala wamekusanyika wampinge Bwana na Masihi wake.’

Read full chapter