Matendo Ya Mitume 4:13-31
Neno: Bibilia Takatifu
Ujasiri Wa Petro Na Yohana Washangaza Watu
13 Wale viongozi na wazee walipoona ujasiri wa Petro na Yohana na kufahamu ya kuwa walikuwa watu wa kawaida wasio na elimu walishangaa sana. Wakatambua kwamba hawa watu walikuwa na Yesu. 14 Lakini kwa kuwa walimwona yule kilema aliyeponywa ame simama nao hawakuweza kusema lo lote kupinga maneno yao. 15 Wakawaamuru watoke nje ya ule ukumbi. 16 Kisha wakaanza kuulizana, “Tuwafanye nini watu hawa? Hatuwezi kukanusha muujiza huu mkubwa walioufanya ambao ni dhahiri kwa kila mtu Yerusalemu. 17 Lakini tunaweza kuzuia jambo hili lisiendelee kuenezwa kwa watu kama tukiwakanya wasiseme tena na mtu ye yote kwa jina la Yesu.” 18 Kwa hiyo wakawaita tena ndani wakawaamuru wasiseme au kufundisha watu tena kwa jina la Yesu.
Bora Kumtii Mungu Kuliko Wanadamu
19 Ndipo Petro na Yohana wakawajibu, “Ninyi amueni wenyewe lililo bora kutenda mbele za Mungu: kuwatii ninyi au kumtii Mungu. 20 Lakini sisi hatuwezi kuacha kusema yale tuliyoyaona na kuyasikia.”
21 Wale viongozi wakawaonya tena kwa vitisho, kisha waka waacha waende. Hawakuona njia ya kuwaadhibu kwa kuwa waliwaogopa wale watu ambao walishuhudia ule muujiza uliotendeka, nao wali kuwa wakimsifu Mungu. 22 Na yule mtu aliyeponywa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka arobaini.
23 Mara Petro na Yohana walipoachiliwa, walirudi kwa waamini wenzao wakawaeleza waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee. 24 Waamini wote waliposikia maneno yao walimwomba Mungu kwa pamoja wakasema, “Wewe Bwana Mtukufu, uliyeumba mbingu na nchi na bahari na kila kiumbe kilichopo, 25 wewe ulitamka kwa njia ya Roho wako mtakatifu kupitia kwa baba yetu Daudi mtumishi wako, aliposema, ‘Mbona mataifa wanaghadhabika, na watu wanawaza mambo yasiyo na maana? 26 Wafalme wa dunia wamejiandaa na watawala wamekusanyika wampinge Bwana na Masihi wake.’ 27 Ndiyo sababu katika mji huu Herode na Pontio Pilato walikutana na Waisraeli wote na watu wa mataifa juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, 28 wakaamua kumfanyia yale yote ambayo wewe ulikuwa umekusudia tangu awali na kupanga kwa uweza wako yatendeke.
29 “Sasa Bwana, sikia vitisho vyao na utuwezeshe sisi wat umishi wako kuhubiri neno lako kwa ujasiri mkuu; 30 na unyooshe mkono wako ili tuweze kuponya wagonjwa na kutenda ishara na miu jiza kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.” 31 Walipokwisha kusali, nyumba waliyokuwa wamekutania ikatikisika na wote wakaja zwa na Roho Mtakatifu, wakahubiri neno la Mungu kwa ujasiri.
Read full chapter
Yohana 16:16-33
Neno: Bibilia Takatifu
Huzuni Na Furaha
16 “Baada ya muda mfupi hamtaniona tena; na kisha muda mfupi baadaye mtaniona.” 17 Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Baada ya muda mfupi hamtaniona tena na muda mfupi baadaye mtaniona’? Na ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa baba’?” 18 Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘muda mfupi?’ Hatuelewi ana maana gani!”
19 Yesu alitambua walilotaka kumwuliza kwa hiyo akawaambia, “Mnaulizana nina maana gani nisemapo, ‘Baada ya muda mfupi ham taniona tena na baada ya muda mfupi mtaniona?’ 20 Ninawaambia yaliyo hakika kwamba mtalia na kuomboleza lakini ulimwengu utafu rahi. Mtahuzunika lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 Mwanamke akaribiapo kuzaa huwa na huzuni kwa sababu saa yake ya uchungu imefika. Lakini mtoto azaliwapo mama anasahau mateso hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto duniani. 22 Na ninyi sasa mna huzuni lakini nitawaona tena na mtafurahi, wala hakuna atakayewaondolea furaha yenu. 23 Wakati huo hamtaniomba kitu cho chote. Ninawaambia kweli kwamba Baba yangu atawapa lo lote mta kaloomba kwa jina langu. 24 Mpaka sasa hamjaomba lo lote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapewa ili furaha yenu ipate kukamil ika.
Ushindi
25 “Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Lakini wakati unakuja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nita waeleza wazi wazi kuhusu Baba yangu. 26 Wakati huo mtaomba kwa jina langu. Wala sisemi kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu; 27 kwa maana Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Baba. 28 Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni, tena sasa naondoka ulimwenguni na ninak wenda kwa Baba.” 29 Wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza wazi wazi wala si kwa mafumbo. 30 Sasa tumejua kwamba wewe una jua mambo yote wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa hiyo tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.” 31 Yesu akawajibu, “Sasa mnaamini? 32 Saa inakuja, tena imeshawadia, ambapo mtata wanyika, kila mtu aende nyumbani kwake na kuniacha peke yangu; lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yuko pamoja nami. 33 Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica