Karibu na pwani ile, kulikuwa na shamba kubwa la gavana wa kisiwa kile aliyeitwa Publio. Huyu gavana alitukaribisha kwa ukarimu mkubwa, akatufanyia sherehe kwa muda wa siku tatu. Baba yake Publio alikuwa mgonjwa amelala, ana homa kali na kuhara damu. Paulo akaenda kumwona, akamwekea mikono akamwombea; naye akapona. Jambo hili lilipotokea, watu wote wa kisiwa kile wal iokuwa wagonjwa wakaja, nao wakaponywa.

Read full chapter