32 Basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua kwenye meli wakaiacha mashua ichukuliwe baharini. 33 Mapambazuko yalipokaribia, Paulo akawasihi watu wote wale chakula akisema, “Leo ni siku ya kumi na nne mmekuwa katika wasiwasi bila kula cho chote. 34 Kwa hiyo nawasihi mle chakula kwa maana mnakihi taji ili muweze kuishi. Hakuna mmoja wenu atakayepoteza hata unywele mmoja kichwani mwake.”

Read full chapter