22 Agripa akasema, “Ningependa nimsikilize mtu huyu mwenyewe.”

Paulo Ajitetea Mbele Ya Agripa

23 Kesho yake Agripa na Bernike walifika kwa fahari kubwa wakaingia katika ukumbi wa mkutano pamoja na mahakimu wa kijeshi na watu mashuhuri wa mji. Ndipo kwa amri ya Festo Paulo akaletwa.

24 Festo akasema, “Mfalme Agripa, na ninyi nyote mlio hapa pamoja nasi leo, mnamwona hapa huyu mtu ambaye Wayahudi wote wa Yerusalemu na wa hapa Kaisaria wamenisihi, wakipiga makelele kwamba hastahili tena kuishi.

Read full chapter