21 isipo kuwa lile jambo nililotangaza wazi wazi nilipojitetea mbele yao, kwamba, ‘Mimi nimeshtakiwa mbele yenu leo kuhusu ufufuo wa wafu.’

22 Ndipo Feliksi ambaye alikuwa anafahamu vizuri habari za Njia, akaamua kuahirishwa kwa kesi, akasema, “Mara jemadari Lisia atakapofika nitatoa hukumu yangu juu ya kesi hii.” 23 Akaamuru askari amweke Paulo kizuizini chini ya ulinzi lakini awe na uhuru kiasi, na marafiki zake wasizuiwe kumhudumia.

Read full chapter