Matendo Ya Mitume 21-28
Neno: Bibilia Takatifu
Paulo Aenda Yerusalemu
21 Tulipokwisha agana nao tuliondoka tukasafiri moja kwa moja, mpaka Kosi, na siku ya pili yake tukafika Rodo, na kutoka huko tukaenda Patara. 2 Hapo tukapata meli iliyokuwa ikielekea Foinike tukaingia ndani tukasafiri nayo. 3 Tulipokaribia kisiwa cha Kipro, tulikizunguka upande wa kushoto, tukasafiri mpaka Siria, tukatia nanga katika bandari ya Tiro ambapo meli yetu ili kuwa ipakue shehena yake. 4 Tukawatafuta waamini wa huko, tukakaa nao kwa siku saba. Wale waamini wakiwa wameongozwa na Roho walim wambia Paulo asiende Yerusalemu. 5 Muda wa kukaa nao ulipokwisha, tuliendelea na safari yetu na wale ndugu waamini pamoja na wake zao na watoto wao walitusindikiza hadi nje ya mji. Wote tulipiga magoti pale pwani tukaomba, kisha tukaagana.
6 Ndipo tukaingia ndani ya meli na wale ndugu wakarudi mak wao. 7 Tuliendelea na safari yetu kutoka Tiro tukafika Tolemai, tukawasalimu waamini wa huko na tukakaa nao kwa siku moja. 8 Kesho yake tuliondoka tukafika Kaisaria. Huko tukaenda nyumbani kwa mwinjilisti mmoja jina lake Filipo ambaye alikuwa kati ya wale watu saba waliochaguliwa kule Yerusalemu, tukakaa kwake. 9 Filipo alikuwa na binti wanne ambao walikuwa bado hawajaolewa nao walikuwa na karama ya unabii. 10 Wakati tulipokuwa huko kwa siku kadhaa, alifika nabii mmoja aitwaye Agabo kutoka Yudea. 11 Alikuja kutuona akachukua mshipi wa Paulo, akautumia kufunga mikono yake mwenyewe na miguu yake akasema, “Roho Mtakatifu anasema: ‘Hivi ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mwe nye mshipi huu na kumkabidhi kwa watu wa mataifa .”’ 12 Tulipo sikia maneno haya sisi na ndugu wengine tulimwomba Paulo asiende Yerusalemu. 13 Lakini Paulo alijibu, “Kwa nini mnanivunja moyo kwa machozi yenu? Mimi niko tayari kufungwa na hata kufa huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu.” 14 Na kwa kuwa hatukuweza kumshawishi asiende, tuliacha kumsihi tukamwambia, “Mapenzi ya Bwana na yatendeke.”
15 Baadaye tulijiandaa tukaondoka kwenda Yerusalemu. 16 Baadhi ya waamini kutoka Kaisaria waliongozana nasi, wakat upeleka nyumbani kwa Mnasoni, mtu wa Kipro, mmoja wa waamini wa zamani, tukae kwake.
Taarifa Ya Paulo Kwa Kanisa La Yerusalemu
17 Tulipofika Yerusalemu ndugu wa huko walitukaribisha kwa furaha. 18 Kesho yake Paulo alikwenda nasi kwa Yakobo, na wazee wote wa kanisa walikuwepo. 19 Baada ya kuwasalimu, Paulo alitoa taarifa kamili ya mambo yote ambayo Mungu alifanya kati ya watu wa mataifa kwa kumtumia yeye. 20 Baada ya maelezo yake wote walimtukuza Mungu. Ndipo wakamwambia, “Unavyoona ndugu, kuna maelfu ya Wayahudi walioamini; nao wote wanaishika sheria kwa bidii. 21 Lakini wamekuwa wakiambiwa habari zako kuwa wewe umew afundisha Wayahudi wanaoishi na watu wa mataifa waache kushika sheria za Musa; na kuwaambia wasitahiri watoto wao, au kufuata mila za Kiyahudi. 22 Sasa tufanyeje? Kwa maana watasikia kwamba umefika Yerusalemu. 23 Kwa hiyo fanya kama tunavyokushauri. Tunao watu wanne hapa ambao wameweka nadhiri. 24 Wachukue hawa ukajitakase pamoja nao na ulipe gharama zao ili wanyoe nywele zao. Kwa njia hii kila mtu atafahamu ya kuwa mambo waliyosikia si ya kweli na kwamba wewe unashika sheria. 25 Lakini wale watu wa mataifa walioamini tumewapelekea barua tukiwaambia kuwa tumeamua wajitenge na kitu cho chote ambacho kimetolewa kwanza kama sadaka kwa miungu ya sanamu na wasinywe damu au kula nyama ya mnyama aliyeuawa kwa kunyongwa. Tena ni lazima wajitenge na uasherati.” 26 Kwa hiyo Paulo akawachukua wale watu na kesho yake akajita kasa pamoja nao. Akaingia ndani ya Hekalu ili akatoe taarifa ya tarehe ambayo siku zao za utakaso zitamalizika na sadaka kutolewa kwa ajili ya kila mmoja wao.
Paulo Akamatwa
27 Zile siku saba zilipokaribia kumalizika, Wayahudi kutoka jimbo la Asia waliokuwa wamemwona Paulo ndani ya hekalu, waka chochea umati mkubwa wa watu wakamkamata Paulo. 28 Wakapiga kelele wakasema, “Ndugu Waisraeli, tusaidieni! Huyu ni yule mtu ambaye anafundisha watu kila mahali wawadharau watu wetu, wazid harau sheria zetu na hata hili Hekalu. Zaidi ya hayo amewaleta Wagiriki katika Hekalu na kuchafua hapa mahali patakatifu!” 29 Walisema hivi kwa sababu walimwona Trofimo, mwenyeji wa Efeso, akiwa mjini na Paulo wakadhani kuwa Paulo alikuwa amemleta Hekaluni . 30 Habari hizi zikawachochea watu wa mji mzima nao wakakimbia pamoja kwa hasira wakamkamata Paulo wakamtoa nje ya Hekalu. Milango ya Hekalu ikafungwa. 31 Walipokuwa wakitaka kum wua, habari zikamfikia Jemadari wa jeshi la askari wa Kirumi kwamba Yerusalemu yote ilikuwa katika hali ya machafuko. 32 Na mara yule jemadari akachukua maofisa wengine wa jeshi pamoja na maaskari wakakimbilia kwenye ile ghasia. Watu walipomwona jema dari na askari wakija, waliacha kumpiga Paulo. 33 Kisha yule jemadari akamkamata Paulo akaamuru afungwe kwa minyororo miwili. Akauliza yeye ni nani na alikuwa amefanya nini. 34 Baadhi ya watu wakapiga kelele wakieleza jambo moja na wengine wakieleza jingine. Yule jemadari alipoona kuwa hawezi kupata ukweli kamili kwa sababu ya zile kelele, akaamuru Paulo apelekwe katika ngome ya jeshi. 35 Basi walipofika penye ngazi, ilibidi askari wambebe Paulo juu juu kwa sababu ya fujo za ule umati wa watu 36 ambao walikuwa wakiwafuata wakipiga kelele, “Mwueni!”
Paulo Anajitetea
37 Walipokuwa wanakaribia kuingia katika ngome ya jeshi, Paulo alimwuliza yule jemadari, “Je, naweza kusema jambo moja?” Yule jemadari akajibu, “Kumbe unajua Kigiriki? 38 Wewe si yule Mmisri ambaye siku za karibuni alianzisha uasi akaongoza majam bazi elfu nne wenye silaha jangwani?” 39 Paulo akajibu, “Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso, jimbo la Kilikia na raia wa mji wenye sifa. Tafadhali niruhusu nizungumze na hawa watu.” 40 Yule jemadari alipomruhusu azungumze, Paulo akasimama penye ngazi akawapungia watu mkono ili wanyamaze. Watu walipokuwa kimya kabisa, Paulo akazungumza nao kwa lugha ya Kiebrania, akasema;
Ushuhuda Wa Paulo Kwa Wayahudi Wa Yerusalemu
22 “Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni utetezi wangu.” 2 Waliposikia akisema kwa lugha ya Kiebrania, wakatulia zaidi, naye akasema, 3 “Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kili kia, lakini nimekulia hapa Yerusalemu, nikiwa mwanafunzi wa Gamalieli. Nilielimishwa kwa kufuata utaratibu maalumu wa sheria za baba zetu, nikiwa na ari ya kumheshimu Mungu kama ninyi mlivyo siku hii ya leo. 4 Niliwatesa wafuasi wa ‘Njia’ mpaka wakafa. Niliwakamata, waume kwa wake, nikawafunga na kuwaweka gerezani. 5 Kuhani mkuu na baraza zima la wazee ni mashahidi wangu kuhusu jambo hili. Wao ndio walionipa barua za kupeleka kwa ndugu zao huko Dameski. Kwa hiyo nilikwenda kuwakamata wafuasi wa ‘Njia’ niwalete Yerusalemu kama wafungwa ili waadhibiwe. 6 Nilipokuwa nimekaribia kufika Dameski, mnamo muda wa kama saa sita mchana, kulitokea mwanga mkali kutoka mbinguni ukaangaza pande zote kuni zunguka. 7 Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, ‘Sauli! Sauli! Mbona unanitesa?’ 8 Nikajibu, ‘Wewe ni nani Bwana?’ Naye akajibu, ‘Mimi ni Yesu wa Nazareti unayemtesa.’
9 “Wale watu niliokuwa nikisafiri nao waliona ule mwanga, lakini hawakuelewa ile sauti ya yule aliyekuwa akisema nami. 10 Nikauliza, ‘Nifanye nini Bwana?’ Naye Bwana akaniambia, ‘Inuka uingie Dameski na huko utaambiwa mambo yote uliyopangiwa kufanya.’ 11 Nilikuwa sioni kwa sababu ya ule mwanga mkali kwa hiyo wenzangu wakanishika mkono wakaniongoza na hivyo tukafika Dameski. 12 “Mtu mmoja aitwaye Anania, mtu wa dini, aliyeshika sana sheria zetu, na ambaye aliheshimiwa sana na Wayahudi wote wa Dameski, 13 alinijia akasimama karibu yangu akasema, ‘Ndugu Sauli, pokea tena uwezo wa kuona!’ Na wakati ule ule nikaweza kuona tena, nikamwona Anania. 14 Akasema, ‘Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe ufahamu mapenzi yake, umwone yeye Mwenye Haki na usikie akisema nawe kwa sauti yake mwenyewe. 15 Kwa kuwa utakuwa shahidi wake kwa watu wote uwaambie yote uliyoyaona na kuyasikia. 16 Sasa basi, mbona unakawia? Simama ubatizwe, ukaoshwe dhambi zako kwa kuliitia jina lake.” ’
Wito Wa Paulo Kuwahubiri Mataifa
17 “Niliporudi Yerusalemu nikawa naomba Hekaluni 18 nilim wona katika ndoto akiniambia ‘Harakisha uondoke Yerusalemu upesi kwa sababu watu hawa hawatakubali ushuhuda wako juu yangu.’ 19 Nikajibu, ‘Bwana, wanajua jinsi nilivyokuwa nikienda katika masinagogi nikawafunga gerezani na kuwapiga wale waliokuamini wewe. 20 Na hata shahidi wako Stefano alipokuwa anauawa mimi nilikuwa nimesimama kando nikikubaliana na kitendo hicho na nikashika mavazi ya wale waliomwua. 21 Akaniambia, ‘Nenda, kwa maana nitakutuma mbali, kwa watu wa mataifa.”
22 Watu walimsikiliza Paulo mpaka hapo; kisha wakapaaza tena sauti zao wakasema, “Mwondosheni duniani! Mtu kama huyu hasta hili kuishi!” 23 Walipoendelea kupiga kelele na kupeperusha nguo zao na kutupa mavumbi juu hewani, 24 yule jemadari akaamuru wale askari wake wamwingize Paulo katika ngome na wamhoji na kum chapa viboko ili aeleze vizuri kwa nini wale Wayahudi walikuwa wanampigia makelele. 25 Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wamchape viboko, Paulo akamwambia askari aliyekuwa karibu naye, “Je, ni halali kumpiga raia wa Kirumi kabla hajahu kumiwa kwa kosa lo lote?” 26 Yule askari aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari akamwuliza, “Unajua unalolifanya? Huyu mtu ni raia wa Kirumi.” 27 Kwa hiyo yule jemadari akaja akamwuliza Paulo, “Niambie, wewe ni raia wa Kirumi?” Paulo aka jibu, “Ndio.” 28 Yule jemadari akasema, “Mimi nilinunua uraia wangu kwa fedha nyingi.” Paulo akamjibu, ‘ ‘Lakini mimi ni Mrumi wa kuzaliwa.” 29 Wale wote waliokuwa wamejiandaa kumhoji wakaondoka haraka haraka na yule jemadari akaingiwa na hofu, kwa maana alitambua ya kuwa alikuwa amemfunga raia wa Kirumi kinyume cha sheria.
Paulo Apelekwa Mbele Ya Baraza
30 Kesho yake yule jemadari alimfungua Paulo zile kamba ali zofungwa akaamuru makuhani wakuu na baraza lote likutane. Akamleta Paulo mbele yao ili apate kujua kwa nini Wayahudi wali kuwa wanamshtaki.
23 Paulo akawakazia macho wajumbe wa baraza, akasema, “Ndugu zangu, mimi nimeishi nikiwa na dhamiri safi kabisa siku zote mbele za Mungu, mpaka leo.” 2 Kuhani mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa karibu na Paulo wampige kofi mdomoni. 3 Ndipo Paulo akasema, “Mungu atakupiga, wewe ukuta uliopakwa chokaa! Unawe zaje kusikiliza kesi hii kwa mujibu wa sheria, na hapo hapo, kinyume cha sheria, unaamuru nipigwe?” 4 Wale watu waliokuwa wamesimama karibu wakamwambia Paulo, “Mbona unamtukana kuhani mkuu wa Mungu?” 5 Paulo akajibu, “Ndugu zangu, sikujua kwamba yeye ni kuhani mkuu. Kwa maana Maandiko yanasema, ‘Usimseme vibaya kiongozi wa watu wako.’ ” 6 Paulo alipotambua ya kuwa baadhi ya wajumbe wa baraza walikuwa Masadukayo na wengine ni Mafarisayo alisema nao kwa sauti kubwa, “Ndugu zangu! Mimi ni Mfarisayo, mtoto wa Mafarisayo; na hapa nimeshitakiwa kuhusu tumaini juu ya ufufuo wa wafu.” 7 Aliposema haya, Mafarisayo na Masadukayo wakafarakana na baraza zima likagawanyika. 8 Kwa maana Masadukayo wanaamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho; lakini Mafarisayo wanaamini haya yote. 9 Kelele zikazidi sana; na baadhi ya waandishi wa sheria wa upande wa Mafarisayo, wakasimama wakiwapinga wengine wakasema, “Hatuoni kosa lo lote alilofanya mtu huyu! Huenda ikawa malaika au roho amezungumza naye kweli!” 10 Mabishano yalipozidi kuwa makali, yule jemadari aliogopa kuwa wangeweza kumrarua Paulo vipande vipande. Kwa hiyo akaamuru askari wakamtoe Paulo alipokuwa, arudishwe kwenye ngome ya jeshi. 11 Usiku uliofuata, Bwana akamtokea Paulo akasimama karibu naye akamwambia, “Jipe moyo! Kama ulivyonishuhudia hapa Yerusalemu, itakubidi unishuhudie na huko Rumi pia.”
Njama Za Wayahudi Kumwua Paulo
12 Kulipopambazuka Wayahudi wakala njama ya kumwua Paulo. Wakaweka nadhiri kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wamemwua Paulo. 13 Waliofanya mpango huu walikuwa zaidi ya watu arobaini. 14 Wakaenda kwa kuhani mkuu na wazee wakasema, “Tumeweka nad hiri ya pamoja kwamba hatutakula wala kunywa mpaka tumwue Paulo. 15 Kwa hiyo ninyi pamoja na baraza, pelekeni ombi kwa jemadari ili Paulo aletwe barazani, mtoe udhuru kwamba mnataka kuchunguza kesi yake kwa usahihi zaidi. Sisi tutakuwa tayari kumwua hata kabla hajakaribia kufika hapa.” 16 Basi kumbe binamu yake Paulo alisikia kuhusu mpango huu. Akaenda katika ngome ya jeshi akamweleza Paulo mambo haya. 17 Paulo akamwita mmoja wa wale maaskari akamwambia, “Mchukue kijana huyu kwa jemadari, ana neno la kumwambia.” 18 Yule askari akamchukua yule kijana mpaka kwa jemadari akamwambia, “Yule mfungwa Paulo aliniita akaniambia nimlete huyu kijana kwako, kwa sababu ana neno la kukuambia.” 19 Yule jemadari akamchukua yule kijana kando akamwuliza, “Unataka kuniambia nini?” 20 Naye akasema, “Wayahudi wameku baliana wakuombe kesho umpeleke Paulo kwenye Baraza lao kwa kisingizio kwamba wanataka kuchunguza kesi yake kwa uangalifu zaidi. 21 Lakini usikubali ombi lao kwa maana zaidi ya watu aro baini wamekula njama kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wamwue Paulo nao wamejiweka tayari kumvizia ukishakubali ombi lao.” 22 Yule jemadari akamruhusu yule kijana aende, akamwonya akisema, “Usimwambie mtu ye yote kwamba umenieleza habari hizi.”
Paulo Apelekwa Kaisaria Kwa Gavana Feliksi
23 Yule jemadari akawaita maaskari wawili akawaambia, “Tay arisheni askari mia mbili watakaokwenda Kaisaria pamoja na askari wa farasi sabini, na askari wa mikuki mia mbili; nanyi muwe tay ari kuondoka leo saa tatu za usiku. 24 Pia tayarisheni na farasi watakaotumiwa na Paulo, mumpeleke salama mpaka kwa gavana Feliksi.” 25 Kisha akaandika barua kwa Feliksi kama ifuatavyo: 26 “Mimi Klaudio Lisia, nakuandikia wewe gavana mtukufu Feliksi. Salamu. 27 Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi wakawa kar ibu kumwua, ndipo mimi nilipofika na askari wangu nikamwokoa kwa kuwa nilipata habari kwamba yeye ni raia wa Kirumi. 28 Nami nikampeleka mbele ya baraza lao ili nipate kujua kosa alilofanya. 29 Ndipo nikagundua ya kuwa alikuwa anashtakiwa kuhusu sheria yao, lakini hakuwa na kosa la kustahili kifo au kifungo. 30 Lakini nilipata habari kwamba kuna mpango wa kumwua nikaamua nimpeleke kwako mara moja, nikawaamuru washitaki wake walete mashtaka yao kwako.” 31 Basi wale askari wakamchukua Paulo usiku wakampeleka mpaka Antipatri kama walivyoamriwa. 32 Kesho yake wakarudi kituoni wakawaacha wale askari wa mikuki waendelee na safari pamoja na Paulo. 33 Walipofika Kaisaria walimpa Liwali ile barua na pia wakamkabidhi Paulo kwake. 34 Alipokwisha soma ile barua, alimwuliza Paulo ametoka jimbo gani. Alipofahamishwa kuwa anatoka Kilikia 35 alisema, “Nitasikiliza kesi yako mara tu washtaki wako watakapofika.” Akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi katika ikulu ya Herode.
Mashtaka Ya Wayahudi Juu Ya Paulo
24 Baada ya siku tano, Kuhani Mkuu Anania akafika pamoja na baadhi ya wazee na wakili mmoja aitwaye Tertulo. Wakatoa mashtaka yao juu ya Paulo mbele ya Gavana. 2 Na Paulo alipoitwa, Tertulo akaanza kutoa mashtaka akasema, “Mtukufu Feliksi, kutokana na uongozi wako wa busara tumekuwa na amani ya kudumu na tunatambua ya kuwa mabadiliko mengi muhimu yaliyotokea katika taifa letu yameletwa na uwezo wako wa kuona mbele. 3 Wakati wote na kila mahali tunapokea mambo haya yote kwa shukrani za dhati. 4 Lakini nisije nikakuchosha, nakuomba kwa hisani yako utusikilize kwa muda mfupi. 5 Tumemwona mtu huyu kuwa ni mfanya fujo ambaye ana chochea maasi kati ya Wayahudi dunia nzima. Yeye ni kiongozi wa dhehebu la Wanazareti. 6 Tena alijaribu kulichafua Hekalu letu lakini tulimkamata [tukataka kumhukumu kwa mujibu wa sheria zetu, 7 lakini jemadari Lisia alikuja akamchukua kutoka kwetu kwa kutu mia nguvu 8 akaamuru wanaomshtaki walete mashtaka yao mbele yako]. Wewe mwenyewe ukimwuliza maswali utathibitisha ukweli wa mashtaka yote tunayoleta mbele yako kumhusu yeye.” 9 Wayahudi wakamwunga mkono wakithibitisha kwamba mashtaka yote yalikuwa ya kweli.
Paulo Ajitetea Mbele Ya Feliksi
10 Gavana Feliksi alipomruhusu Paulo ajitetee, yeye alisema, “Najua kwamba wewe umekuwa hakimu katika taifa hili kwa miaka mingi kwa hiyo natoa utetezi wangu bila wasi wasi. 11 Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipokwenda Yerusalemu kuabudu. 12 Hawa wanaonish taki hawakunikuta nikibishana na mtu ye yote au nikianzisha fujo katika Hekalu au katika sinagogi au mahali pengine po pote mjini. 13 Wala hawawezi kabisa kuthibitisha mambo haya wanayon ishtaki. 14 Lakini nakiri mbele yako kuwa mimi namwabudu Mungu wa baba zetu kwa kufuata ile ‘Njia’ ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kilichoandikwa katika Sheria ya Musa na Mana bii 15 na ninalo tumaini kwa Mungu ambalo hata na wao wanaliku bali, kwamba kutakuwa na ufufuo wa wote, walio na haki na wasio na haki. 16 Kwa hiyo ninafanya kila jitihada kuishi nikiwa na dhamiri safi mbele za Mungu na mbele za wanadamu. 17 Basi, baada ya kuwa nje ya Yerusalemu kwa miaka kadhaa nilikuja mjini kuwale tea watu wa taifa langu sadaka kwa ajili ya maskini na kutoa dha bihu. 18 Nilikuwa nimeshatakaswa waliponikuta Hekaluni nikifanya mambo haya, na hapakuwa na umati wa watu wala fujo yo yote. 19 Lakini kulikuwa na Wayahudi kutoka Asia, nadhani nao walista hili wawepo hapa mbele yako ili watoe mashtaka yao kama wanalo lo lote la kunishtaki. 20 La sivyo, watu hawa waseme ni kosa gani walilogundua nimefanya niliposhtakiwa mbele ya Baraza, 21 isipo kuwa lile jambo nililotangaza wazi wazi nilipojitetea mbele yao, kwamba, ‘Mimi nimeshtakiwa mbele yenu leo kuhusu ufufuo wa wafu.’
22 Ndipo Feliksi ambaye alikuwa anafahamu vizuri habari za Njia, akaamua kuahirishwa kwa kesi, akasema, “Mara jemadari Lisia atakapofika nitatoa hukumu yangu juu ya kesi hii.” 23 Akaamuru askari amweke Paulo kizuizini chini ya ulinzi lakini awe na uhuru kiasi, na marafiki zake wasizuiwe kumhudumia. 24 Baada ya siku chache Feliksi akaja na mkewe Drusila ambaye alikuwa Myahudi. Akatuma Paulo aitwe, wakamsikiliza akizungumza juu ya kumwamini Kristo Yesu. 25 Na Paulo alipokuwa akiwaeleza juu ya kuwa na kiasi na juu ya hukumu ya mwisho, Feliksi aliin giwa na hofu akasema, “Tafadhali sasa nenda, nitakuita tena nikipata nafasi.” 26 Wakati huo huo Feliksi alitazamia kwamba Paulo angempatia hongo, kwa hiyo akawa anamwita mara kwa mara kuzungumza naye. 27 Lakini baada ya miaka miwili kupita, Porkio Festo akachukua nafasi ya Feliksi kama Gavana; na kwa sababu Feliksi alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, akamwacha Paulo gere zani.
Paulo Anajitetea Mbele Ya Festo
25 Siku tatu baada ya Festo kuwasili Kaisaria kuanza kazi, alisafiri kwenda Yerusalemu. 2 Makuhani wakuu na viongozi wa Way ahudi wakamletea mashtaka yao juu ya Paulo, na wakamwomba Festo 3 awafanyie upendeleo, amrudishe Paulo Yerusalemu; wakiwa na mpango wa kumwua Paulo njiani. 4 Festo akawajibu, “Paulo yuko kizuizini huko Kaisaria, na mimi natarajia kwenda huko hivi kari buni. 5 Kwa hiyo tumeni viongozi wenu tuongozane pamoja na kama huyu mtu amefanya kosa lo lote, wao walete mashtaka yao.” 6 Festo alikaa nao kwa muda wa siku nane au kumi kisha akaondoka kwenda Kaisaria. Kesho yake akakaa katika baraza la mahakama, akaamuru Paulo aletwe. 7 Paulo alipoletwa, wale Wayahudi wal iotoka Yerusalemu walisimama wakaanza kutoa mashtaka mengi mazito ambayo hawakuweza kuyathibitisha. 8 Lakini Paulo alijitetea, akasema, “Sikufanya jambo lo lote kinyume cha sheria za Wayahudi au Hekalu au kinyume cha Kaisari. ” 9 Festo akitaka kuwapendeza Wayahudi, alimwuliza Paulo, “Je, ungependa kwenda Yerusalemu ukahojiwe huko kuhusu mashtaka haya mbele yangu?” 10 Paulo akasema, “Mimi nasimama mbele ya baraza la mahakama ya Kaisari. Baraza hili ndilo lina wajibu wa kusikiliza kesi hii. Kama unav yojua sijawatendea Wayahudi uovu wo wote. 11 Kama mimi ni mhal ifu na nimetenda kosa linalostahili hukumu ya kifo, sijitetei ili nisiuawe; lakini kama mashtaka yao juu yangu hayana msingi, hakuna mtu atakayeweza kunitia mikononi mwao waniue. Ninakata rufaa, kesi yangu isikilizwe na Kaisari.” 12 Festo akajadiliana na baraza kisha akasema, “Umeomba rufaa usikilizwe na Kaisari; basi utakwenda kwa Kaisari.”
Paulo Afikishwa Mbele Ya Mfalme Agripa
13 Baada ya siku chache mfalme Agripa na Benike wakafika Kaisaria kumkaribisha Festo. 14 Kwa kuwa walikuwa wanakaa Kais aria kwa muda mrefu, Festo alipata nafasi ya kujadiliana na mfalme kesi ya Paulo; akamwambia, “Kuna mtu mmoja hapa ambaye Feliksi alimwacha gerezani kama mfungwa. 15 Nilipokwenda Yerus alemu, makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi walileta mashtaka yao juu yake wakitaka ahukumiwe. 16 Lakini mimi niliwaambia kwamba sheria za Kirumi haziruhusu kumhukumu mtu aliyeshitakiwa kabla hajapata nafasi ya kukutana uso kwa uso na washitaki wake naye apewe nafasi ya kujitetea. 17 Walipofika hapa pamoja nami, siku kawia, bali nilikaa pamoja na baraza la mahakama nikaamuru mshta kiwa aletwe. 18 Lakini washtaki wake waliposimama, hawakutaja aina yo yote ya uhalifu kama nilivyotarajia, 19 bali walikuwa na mashtaka kuhusu mabishano fulani juu ya dini yao na juu ya mtu aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo alidai kwamba anaishi. 20 Sikujua jinsi ya kuchunguza mambo haya kwa hiyo nikamwuliza Paulo kama angelipenda kwenda Yerusalemu mashtaka haya yakasiki lizwe huko. 21 Lakini Paulo alipokata rufaa, akaomba akae kizuizini mpaka Kaisari atakapotoa uamuzi wake, niliamuru awekwe rumande mpaka nitakapompeleka kwa Kaisari.” 22 Agripa akasema, “Ningependa nimsikilize mtu huyu mwenyewe.”
Paulo Ajitetea Mbele Ya Agripa
23 Kesho yake Agripa na Bernike walifika kwa fahari kubwa wakaingia katika ukumbi wa mkutano pamoja na mahakimu wa kijeshi na watu mashuhuri wa mji. Ndipo kwa amri ya Festo Paulo akaletwa.
24 Festo akasema, “Mfalme Agripa, na ninyi nyote mlio hapa pamoja nasi leo, mnamwona hapa huyu mtu ambaye Wayahudi wote wa Yerusalemu na wa hapa Kaisaria wamenisihi, wakipiga makelele kwamba hastahili tena kuishi. 25 Lakini mimi sikuona kosa lo lote alilotenda linalostahili hukumu ya kifo; na kwa kuwa yeye mwenyewe amekata rufaa kesi yake isikilizwe na Kaisari, niliamua nimpeleke kwake. 26 Lakini sina mapendekezo kamili ya kumwandi kia mtukufu Kaisari juu ya huyu mshtakiwa. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu na hasa mbele yako wewe mfalme Agripa ili baada ya kumhoji mshtakiwa nipate jambo la kuandika. 27 Kwa maana ita kuwa si jambo la busara kumpeleka mfungwa kwa Kaisari bila kuon yesha wazi wazi mashtaka yanayomkabili.”
26 Mfalme Agripa akamwambia Paulo, “Unayo ruhusa kujite tea.” Paulo akanyoosha mkono wake, akaanza kujitetea akasema,
2 “Mfalme Agripa, najiona kuwa mwenye bahati kwamba ninatoa utetezi wangu mbele yako kuhusu mashtaka yote ya Wayahudi. 3 Kwa sababu nafahamu ya kuwa wewe unajua kwa undani mila na maswala yote ya mabishano kati ya Wayahudi. Kwa hiyo nakusihi unisikilize kwa uvumilivu.
4 “Wayahudi wote wanajua jinsi nilivyoishi kutoka utotoni, kwa maana tangu mwanzo wa maisha yangu niliishi katika nchi yangu na pia Yerusalemu. 5 Pia wamefahamu wakati wote, na wanaweza kushuhudia, ya kuwa nililelewa na kuishi kama Mfarisayo nikifuata masharti halisi ya madhehebu ya dini yetu. 6 Na hata sasa nasi mama hapa nikiwa nashtakiwa kwa sababu nashikilia tumaini ambalo Mungu aliwaahidi baba zetu. 7 Ahadi hii ndio inawafanya makabila kumi na mawili ya Israeli wamwabudu Mungu kwa bidii usiku na mchana wakitarajia kuipokea. Mtukufu Mfalme, ni kwa ajili ya tumaini hili Wayahudi wamenishtaki! 8 Sijui ni kwa nini watu wanadhani ni jambo la ajabu lisilowezekana, kwamba Mungu anawafu fua wafu.
9 Mimi mwenyewe nilikuwa nimeamini kabisa kwamba sina budi kufanya kila niwezalo kupinga jina la Yesu wa Nazareti. 10 Nami ndivyo nilivyofanya kule Yerusalemu. Nilipewa mamlaka na makuhani wakuu, nikawatia kifungoni watakatifu wengi na walipokuwa wakihu kumiwa kuuawa mimi nilipiga kura kuunga mkono hukumu hiyo. 11 Pia niliwaadhibu mara nyingi katika masinagogi nikajaribu kuwalazimisha wakane imani yao. Nilikuwa nimejawa na ghadhabu juu yao nikawafuatilia na kuwatesa hata katika miji ya mbali.
12 “Nilikuwa katika mojawapo ya safari hizi nikielekea Dameski, nikiwa na kibali na amri kutoka kwa makuhani wakuu. 13 Mtukufu Mfalme, nilipokuwa njiani, mnamo saa sita mchana, niliona mwanga mkali kuliko wa jua kutoka mbinguni, ukaniangazia mimi na wale niliokuwa nao, pande zote. 14 Na wote tulipokuwa tumeanguka chini nilisikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kie brania, ‘Sauli, Sauli! Mbona unanitesa? Unajiumiza mwenyewe.’ 15 Nikauliza, ‘Ni nani wewe Bwana?’ Naye akasema, ‘Mimi ni Yesu unayenitesa. 16 Lakini sasa inuka usimame, kwa maana nimejidhi hirisha kwako ili nikuteue uwe mtumishi wangu, ukawaambie wengine mambo yote uliyoyaona kwangu leo, na yale nitakayokuonyesha baad aye. 17 Nitakuokoa kutoka kwa watu wako na watu wa mataifa. 18 Ninakutuma ukawafungue macho yao ili watoke kwenye giza waingie nuruni na watoke katika nguvu za shetani wamgeukie Mungu; ili wapokee msamaha wa dhambi na wapate nafasi pamoja na wote ambao wanatakaswa kwa kuniamini.’
19 Kwa hiyo mtukufu Agripa, sikuweza kuacha kutii haya maagizo ya maono kutoka mbinguni, 20 bali niliwahubiria kwanza watu wa Dameski kisha Yerusalemu na nchi yote ya Yudea na watu wa mataifa mengine pia. Niliwahimiza watubu dhambi zao wamgeukie Mungu na kuishi maisha yanayodhihirisha kwamba kweli wametubu. 21 Ni kwa sababu hii Wayahudi walinikamata nilipokuwa Hekaluni, wakataka kuniua. 22 Lakini mpaka wakati huu nimepata msaada uto kao kwa Mungu, na kwa hiyo nasimama hapa nikitoa ushuhuda wangu kwa watu wote, wakubwa kwa wadogo. Nami sisemi lo lote ila yale ambayo Musa na manabii walitabiri yangetokea: 23 kwamba Kristo atateswa naye kwa kuwa atakuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu, atatangaza mwanga wa wokovu kwa Wayahudi na watu wa mataifa.”
24 Paulo alipofikia hapa katika utetezi wake Festo aliin gilia kati akasema kwa sauti kubwa, “Paulo, umeehuka! Kusoma sana kumekufanya uehuke !” 25 Lakini Paulo akajibu, “Mimi si mwehu, Mtukufu Festo, bali nasema yale yaliyo kweli na ya kuami nika. 26 Mfalme Agripa anajua habari za mambo haya, ndio sababu najieleza wazi wazi mbele yake. Kwa sababu ninahakika kuwa yeye aliyaona mambo haya kwa kuwa hayakufichwa pembeni. 27 Mfalme Agripa, Unawaamini manabii? Ninajua kwamba unaamini.” 28 Kisha Agripa akamjibu, “Unadhani kuwa kwa muda huu mfupi unaweza kuni fanya nikubali kuwa mkristo!” 29 Paulo akasema, “Singejali kama ni kwa muda mfupi au mrefu, lakini shauku yangu ni kwamba wewe na wote wanaonisikiliza leo muwe kama mimi nilivyo, isipo kuwa tu hii minyororo.’ ’ 30 Ndipo Mfalme akasimama na Gavana na Bernike na wengine wote waliokuwa wameketi nao wakasimama. 31 Na walipokuwa faraghani pamoja wakasema, “Mtu huyu hafanyi jambo lo lote linalostahili kifo au kifungo.” 32 Agripa akamwambia Festo, “Mtu huyu angeweza kuachiliwa huru kama hakuwa amekata rufaa kesi yake isikilizwe na Kaisari.”
Paulo Asafirishwa Kwenda Rumi
27 Ilipoamuliwa kwamba twende Italia, walimkabidhi Paulo na wafungwa wengine kwa askari mmoja aitwaye Juliasi ambaye alikuwa wa kikosi cha Kaisari Agusto. 2 Tulipakia meli iliyotoka Adrami tio ambayo ilikuwa ikielekea kwenye bandari zilizopo pwani ya Asia. Tukaanza safari yetu tukiongozana na Aristarko, Mmakedonia wa kutoka Thesalonike. 3 Kesho yake tulifika Sidoni. Juliasi akamfanyia wema Paulo, akamruhusu aende kuwaona rafiki zake wam hudumie. 4 Kutoka huko tuliendelea na safari yetu, na kwa kuwa tulikuwa tunakabili upepo, tukapitia upande wa kisiwa cha Kipro usioelekea upepo. 5 Tukavuka bahari, kutoka upande wa Kilikia, na Pamfilia, tukafika Mira, katika jimbo la Likia. 6 Yule askari akapata meli iliyokuwa inatoka Aleksandria ikielekea Italia, akatupakia humo. 7 Tukasafiri pole pole kwa siku nyingi, na kwa shida na hatimaye tukafika karibu na bandari ya Nido. Lakini kwa kuwa upepo mkali ulikuwa ukivuma kutoka tulikokuwa tukielekea, hatukuweza kuendelea moja kwa moja na safari yetu, bali tulipitia upande wa pili wa Krete tukaizunguka ncha ya Salmone. 8 Baada ya kuizunguka kwa shida tulifika sehemu iitwayo Bandari Nzuri, kar ibu na mji wa Lasea.
9 Tulikuwa tumepoteza muda mrefu baharini na kwa wakati huu safari ilikuwa ya hatari kwa maana majira ya kufunga yalikuwa yamekwisha pita. Paulo akawaonya marubani wa ile meli akasema, 10 ‘ ‘Mabwana, naona tukiendelea na safari hii patatokea maafa na hasara kubwa kwa meli na shehena na hata maisha yetu yatakuwa hatarini.” 11 Lakini yule askari akaamua kusikiliza zaidi ushauri wa nahodha na mwenye meli kuliko maneno ya Paulo. 12 Kwa kuwa ile bandari ilikuwa haifai kukaa wakati wa majira ya baridi, wengi wakashauri kwamba waendelee na safari na pengine kwa bahati wangeweza kufika Foinike. Hii ni bandari iliyoko katika kisiwa cha Krete na ambayo inatazama upande wa kusini-magharibi na kas kazini-magharibi, kwa hiyo wangeweza kukaa huko mpaka majira ya baridi yaishe.
Dhoruba Baharini
13 Upepo ulipoanza kuvuma taratibu toka kusini, wakadhani kuwa hii ilikuwa ni dalili nzuri kwamba wangeweza kuendelea na safari. Kwa hiyo wakang’oa nanga wakasafiri wakipita kando kando ya pwani ya kisiwa cha Krete. 14 Lakini baada ya muda mfupi upepo mkali uitwao ‘Kaskazi-mashariki’ ukavuma toka nchi kavu; 15 ukaipiga ile meli, na kwa kuwa haikuwa rahisi kushindana nao, tukaiachilia meli isukumwe kuelekea kule upepo unakokwenda. 16 Hatimaye tukasafiri kupitia nyuma ya kisiwa kidogo kiitwacho Kauda, ambapo kwa kuwa tulikuwa tumekingiwa upepo na hicho kisiwa, tuliweza kwa shida kuifunga mashua ya kuokolea watu. 17 Watu walipokwisha ivuta mashua hiyo wakaiingiza katika meli, waliifunga kwa kamba kwenye meli. Kisha, kwa kuogopa kwamba wangesukumwa na upepo mkali na kukwama kwenye mchanga karibu na pwani ya Sirti, walishusha matanga wakaiacha meli ielee. 18 Kesho yake dhoruba kali iliendelea kuvuma, kwa hiyo wakaanza kuitupa shehena baharini. 19 Siku ya tatu wakaanza kutupa vifaa vya meli baharini kwa mikono yao wenyewe. 20 Kwa siku nyingi hatukuona jua wala nyota, na dhoruba kali ilikuwa inaendelea kuvuma. Kwa hiyo tukakata tamaa kabisa kwamba tungeokolewa.
21 Kwa kuwa walikuwa wamekaa siku kadhaa bila kula cho chote, Paulo akasimama kati yao akasema, “Mngenisikiliza wala msingeondoka Krete na kupata mkasa huu na hasara hii. 22 Lakini sasa nawaomba mjipe moyo. Hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake ila meli hii itaangamia. 23 Jana usiku, malaika wa Mungu wangu ambaye mimi namwabudu alisimama karibu yangu 24 akasema, ‘Usiogope Paulo; huna budi kujitetea katika kesi yako mbele ya Kaisari; na kwa neema yake, Mungu amekupa maisha ya watu wote wanaosafiri pamoja na wewe.’ 25 Kwa hiyo muwe na matu maini kwa maana nina imani kwa Mungu kwamba mambo yatakuwa kama nilivyoambiwa. 26 Lakini hata hiyo meli yetu itakwama kwenye kisiwa fulani. ”
27 Siku ya kumi na nne, mnamo saa sita za usiku, tulipokuwa bado tunasukumwa na upepo katika bahari ya Adria, mabaharia wali hisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu. 28 Kwa hiyo wakapima kina cha bahari wakakuta kilikuwa mita thelathini na tano hivi, na baada ya kitambo kidogo wakapima tena wakapata kina cha mita ishirini na sita hivi. 29 Wakaogopa kwamba meli yetu ingegonga kwenye miamba, kwa hiyo wakashusha nanga nne nyuma ya meli, wakawa wanaomba kupambazuke. 30 Mabaharia walikuwa wanataka kutoroka kutoka mle melini, wakashusha mashua baharini wakidanga nya kuwa walikuwa wanakwenda kuweka nanga upande wa mbele ya meli. Ndipo 31 Paulo akawaambia wale maaskari na maofisa wao, “Hawa watu wasipobaki katika meli, hamtaweza kuokolewa.” 32 Basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua kwenye meli wakaiacha mashua ichukuliwe baharini. 33 Mapambazuko yalipokaribia, Paulo akawasihi watu wote wale chakula akisema, “Leo ni siku ya kumi na nne mmekuwa katika wasiwasi bila kula cho chote. 34 Kwa hiyo nawasihi mle chakula kwa maana mnakihi taji ili muweze kuishi. Hakuna mmoja wenu atakayepoteza hata unywele mmoja kichwani mwake.” 35 Baada ya maneno haya, Paulo akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega akaanza kula. 36 Ndipo wote wakatiwa moyo, wakaanza kula chak ula. 37 Ndani ya meli tulikuwa jumla ya watu mia mbili na sabini na sita. 38 Baada ya wote kula chakula cha kutosha, wakapunguza uzito wa meli kwa kutupa ngano baharini.
39 Kulipokucha, mabaharia hawakuitambua ile nchi, lakini waliona ghuba yenye ufuko wa mchanga ambako walitaka waielekeze meli kama ingewezekana, ili wafike pwani. 40 Kwa hiyo wakatupa nanga zote baharini, wakalegeza kamba zilizokuwa zikishikilia usukani wa meli, na kutweka tanga la mbele lishike upepo na kuisukuma meli kuelekea pwani. 41 Lakini ile meli ikagonga mwamba ikakwama kwenye mchanga na upande wa mbele wa meli uka banwa kwenye mwamba wala usingeweza kuondolewa tena. Na upande wa nyuma ulivunjika vipande kwa nguvu ya yale mawimbi. 42 Wale askari walikuwa wamepanga kuwaua wafungwa wote ili wasije wakaogelea hadi pwani na kutoroka. 43 Lakini yule Ofisa wa maas kari alitaka kumwokoa Paulo, kwa hiyo akawazuia wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, na waogelee kuelekea pwani; 44 na wengine wajishikize kwenye vipande vya meli waelee navyo. Kwa jinsi hii, watu wote waliokolewa wakafika nchi kavu. 28 1 Tulipofika salama nchi kavu, tuligundua kwamba tuko katika kisiwa kiitwacho Melita. 2 Wenyeji wa kisiwa hicho walitufanyia ukarimu wa ajabu, wakawasha moto na kutukaribisha kwa maana mvua ilikuwa inanyesha na kulikuwa na baridi kali. 3 Paulo alikuwa amekusanya kuni nyingi na alipokuwa akiziweka kwenye moto, aka toka humo nyoka mwenye sumu akikimbia ule moto akajisokotea kwe nye mkono wa Paulo. 4 Wale wenyeji walipomwona yule nyoka ameji sokota kwenye mkono wa Paulo, wakaambiana, “Bila shaka mtu huyu ni muuaji, ijapokuwa ameokoka kufa maji baharini, haki haikumru husu aishi.” 5 Lakini Paulo akamkung’utia yule nyoka ndani ya moto wala yeye hakupata madhara yo yote. 6 Wakangojea wakitarajia kwamba atavimba au ataanguka ghafla na kufa. Lakini baada ya kungoja kwa muda mrefu na hawakuona dalili yo yote mbaya ikimto kea, wakabadili mawazo yao, wakasema yeye ni mungu.
7 Karibu na pwani ile, kulikuwa na shamba kubwa la gavana wa kisiwa kile aliyeitwa Publio. Huyu gavana alitukaribisha kwa ukarimu mkubwa, akatufanyia sherehe kwa muda wa siku tatu. 8 Baba yake Publio alikuwa mgonjwa amelala, ana homa kali na kuhara damu. Paulo akaenda kumwona, akamwekea mikono akamwombea; naye akapona. 9 Jambo hili lilipotokea, watu wote wa kisiwa kile wal iokuwa wagonjwa wakaja, nao wakaponywa. 10 Kwa hiyo wakatuletea zawadi nyingi, nasi tulipokuwa tukijiandaa kuondoka walitupatia kila kitu tulichohitaji kwa ajili ya safari.
Paulo Anawasili Rumi
11 Baada ya miezi mitatu tuliondoka kwa meli iliyokuwa ime toka Aleksandria ikawa imetia nanga katika kisiwa cha Melita mpaka majira ya baridi yaishe. Meli hiyo ilikuwa na picha ya miungu pacha Kasta na Poluksi. 12 Kituo chetu cha kwanza kili kuwa Sirakusa ambako tulikaa kwa siku tatu. 13 Kutoka huko tuka zunguka tukafika Regio; na baada ya siku moja, upepo mkali uka vuma kutoka kusini, na siku ya pili tukafika Puteoli. 14 Na hapa tuliwakuta waamini ambao walitukaribisha tukae nao kwa siku saba. Ndipo tukaendelea na safari mpaka tukafika Rumi. 15 Ndugu waamini wa Rumi walipopata habari zetu, walikuja mpaka soko la Apio na wengine wakaja mpaka mahali paitwapo ‘Mikahawa Mitatu’ kutulaki. Paulo alipowaona, alimshukuru Mungu akachangamka.
Copyright © 1989 by Biblica