Paulo Aenda Makedonia na Ugiriki

20 Fujo zilipokwisha, Paulo aliwaita wanafunzi pamoja akawa tia moyo halafu akawaaga. Akaanza safari yake ya kwenda Makedo nia. Alipokuwa akisafiri, aliwapa waamini katika sehemu zote alizopita maneno ya kuwatia moyo, ndipo akaenda Ugiriki ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa akijiandaa kwenda Siria kwa meli, iligundulika kwamba Wayahudi walikuwa na mpango wa kumwua, kwa hiyo akaamua kurudi akipitia Makedonia. Watu waliofuatana naye safarini ni Sopatro Piro mwenyeji wa Beroya , Aristako na Sekundo kutoka Thesalonike, Gayo mwenyeji wa Derbe; Timotheo, Tikiko na Trofimo wenyeji wa Asia. Hawa walitutangu lia wakaenda kutungojea Troa. Sisi tuliondoka baada ya sikukuu ya mikate isiyotiwa hamira tukasafiri kwa meli na kuungana nao siku tano baadaye huko Troa ambako tulikaa kwa siku saba.

Paulo Akutana Na Waamini Wa Troa

Jioni siku ya kwanza ya Juma tulikuwa tumekutana pamoja kwa chakula na Paulo akaongea nao akiwa na mpango wa kuondoka kesho yake; akaendelea na mazungumzo mpaka usiku wa manane. Chumba cha ghorofani walipokuwa wakikutania kilikuwa na taa nyingi na kijana mmoja jina lake Eutiko alikuwa amekaa dirishani. Paulo alivyoendelea kuongea kijana huyu alizidi kusinzia. Hatimaye alishikwa na usingizi kabisa, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu, akadhaniwa kuwa amekufa. 10 Lakini Paulo alishuka chini akainama, akamkumbatia yule kijana akasema, “Msiwe na hofu, yun gali hai.” 11 Paulo akarudi ghorofani na alipokwisha kula, akaongea nao tena mpaka alfajiri ndipo akaondoka. 12 Yule kijana alichukuliwa nyumbani akiwa hai na wote waliokuwepo walifarijika.

Paulo Atoka Troa Kwenda Mileto

13 Tuliingia katika meli tukasafiri mpaka Aso ambako tuli tarajia kumchukua Paulo kwa maana alikuwa amepanga kusafiri nchi kavu mpaka huko. 14 Alipotukuta huko Aso, tulimchukua melini tukasafiri wote mpaka Mitilene. 15 Kutoka Mitilene tuliendelea kwa meli na kesho yake tukafika pwani ya upande wa pili wa Kio. Siku iliyofuata tukafika Samo na kesho yake tukawasili Mileto. 16 Paulo alikuwa ameamua tusipitie Efeso ili asitumie muda mwingi katika jimbo la Asia; kwa sababu alitaka kama ikiwezekana afike Yerusalemu kabla ya siku ya Pentekoste.

Paulo Anawaaga Wazee Wa Kanisa La Efeso

17 Paulo akiwa Mileto, alituma ujumbe kwenda Efeso kuwaita wazee wa kanisa wakutane naye. 18 Walipofika aliwaambia, “Ninyi mnajua jinsi nilivyoishi nanyi tangu siku ya kwanza nilipofika Asia. 19 Nilimtumikia Bwana kwa unyenyekevu na machozi na kwa mateso yaliyotokana na njama za Wayahudi. 20 Mnajua jinsi ambavyo sikusita kuwaambia cho chote ambacho kingekuwa cha faida kwenu, na jinsi nilivyofundisha hadharani na nyumba kwa nyumba 21 nikiwashuhudia Wayahudi na Wagiriki juu ya kutubu dhambi kwa Mungu na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo. 22 Na sasa nimevutwa na Roho niende Yerusalemu na sijui mambo yatakayonipata huko. 23 Ila katika kila mji niliopitia, Roho Mtakatifu amenifunulia kwamba mbele yangu kifungo na mateso vinaningoja. 24 Lakini nay ahesabu maisha yangu kuwa si kitu cha thamani kwangu, ili mradi niweze kukamilisha wito na kazi niliyopewa na Bwana Yesu; kazi ya kuwashuhudia watu kuhusu Habari Njema ya neema ya Mungu. 25 Na sasa najua ya kuwa hakuna hata mmoja wenu, ninyi ambao kati yenu nimekuwa nikihubiri juu ya Ufalme wa Mungu, atakayeniona tena. 26 Kwa hiyo nawashuhudia wazi leo hii kwamba sina lawama juu ya mtu ye yote kati yenu, 27 kwa sababu sikuacha kuwatangazia mpango kamili wa Mungu. 28 Jilindeni nafsi zenu, na mlinde kundi lote la kondoo ambalo Roho Mtakatifu ameliweka chini ya uongozi wenu; mtunze kanisa la Mungu ambalo amelinunua kwa damu ya Mwa nae. 29 Najua kwamba nikishaondoka, mbwa mwitu wakali watakuja kati yenu nao hawatakuwa na huruma yo yote juu ya kundi lenu. 30 Na hata kati yenu ninyi patatokea watu watakaosema maneno ya kupotosha ili wawavute baadhi ya wanafunzi wawafuate. 31 Kwa hiyo muwe macho; mkumbuke jinsi nilivyomwonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana kwa muda wa miaka mitatu. 32 Na sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake ambalo linaweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi pamoja na wote ambao wameta kaswa. 33 Sikutamani fedha au dhahabu au nguo za mtu ye yote. 34 Ninyi wenyewe mnajua kwamba kwa mikono yangu nimefanya kazi nikapata mahitaji yangu na ya wenzangu. 35 Katika kila jambo nimewaonyesha kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii mtaweza kuwa saidia walio dhaifu, mkikumbuka maneno aliyosema Bwana Yesu kwamba, ‘Kuna baraka kubwa zaidi katika kutoa kuliko kupokea.”’

36 Paulo alipomaliza kusema haya alipiga magoti akaomba pamoja nao wote. 37 Na wote wakalia, wakamkumbatia Paulo na kum busu, 38 wakihuzunika kwa sababu ya maneno aliyowaambia kwamba hawatamwona tena. Wakamsindikiza wakamfikisha kwenye meli.