29 Kwa kuwa sisi ni wa uzao wa Mungu hatupaswi kudhani kuwa yeye ni kama sanamu ya dhahabu au fedha au jiwe iliyotengenezwa kwa akili na ufundi wa mwanadamu. 30 Mungu alisamehe ujinga huo wa zamani, lakini sasa anaamuru watu wote watubu, waachane na miungu ya sanamu. 31 Kwa kuwa amepanga siku ambayo atahukumu ulimwengu kwa haki akimtumia mtu aliyemchagua, ambaye amemhakikisha kwa watu wote kwa kumfufua kutoka kwa wafu.”

Read full chapter