Kwa hiyo wakaendelea na safari kupitia Misia, wakafika Troa. Usiku huo Paulo akaona katika ndoto, mtu wa Makedonia amesimama akimsihi, “Njoo Makedo nia ukatusaidie.” 10 Mara baada ya Paulo kuona maono haya, tulijiandaa kuondoka kwenda Makedonia kwa sababu tuliona kuwa Mungu ametuita kuhubiri Habari Njema kwa watu wa huko.

Read full chapter