12 Kutoka huko tukaende lea na safari hadi Filipi, mji mkuu wa Makedonia ambao ni koloni la Kirumi. 13 Tulikaa Filipi kwa siku chache na siku ya sabato tukaenda nje ya mji kando ya mto, mahali ambapo tulidhani pange faa kwa maombi. Tukakaa chini tukaongea na baadhi ya wanawake waliokuja pale mtoni. 14 Mmoja wa wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mwenyeji wa mji wa Thiatira na mfanya biashara wa nguo za zambarau. Yeye alimpenda Mungu na Bwana akaufungua moyo wake akapokea mahubiri ya Paulo. 15 Basi alipokwisha kubatizwa yeye na jamaa yake, alitusihi akisema, “Kama mmenipokea kweli kama mwamini, tafadhali njooni mkae nyumbani kwangu.” Akatushaw ishi twende naye.

Paulo Na Sila Wafungwa Gerezani

16 Siku moja tulipokuwa tukienda mahali pa sala tulikutana na msichana mmoja mtumwa aliyekuwa na pepo wa kutabiri mambo yaj ayo. Alikuwa amewapatia mabwana wake faida kubwa kwa kutumia uwezo wa kutabiria watu mambo yajayo. 17 Basi alimfuata Paulo na sisi akipiga kelele, “Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye Juu kuliko wote. Wao wanatangaza kwenu njia ya wokovu.” 18 Na aliendelea kusema maneno haya kwa siku nyingi. Lakini Paulo aliudhika, akageuka na kumwambia yule pepo, “Ninakuamuru katika jina la Yesu Kristo, umtoke!” Yule pepo akamtoka wakati ule ule. 19 Basi mabwana wa yule msichana mtumwa walipoona kuwa matumaini yao ya kuendelea kujipatia fedha yametoweka, wakawakamata Paulo na Sila wakawapeleka sokoni mbele ya viongozi wa mji. 20 Waka washtaki kwa mahakimu wakisema, “ Hawa watu ni Wayahudi nao wan aleta fujo mjini kwetu. 21 Wanafundisha desturi ambazo si halali kwetu kama raia wa Kirumi kuzikubali au kuzitimiza.” 22 Umati wa watu waliokuwepo wakaunga mkono mashtaka haya, na wale maha kimu wakatoa amri Paulo na Sila wavuliwe nguo wachapwe viboko. 23 Baada ya kuchapwa sana wakatupwa gerezani, na askari jela akaamriwa aweke ulinzi mkali. 24 Yule askari jela alipopokea amri hiyo akawaweka katika chumba cha ndani mle gerezani na kisha akafunga miguu yao kwa mkatale. 25 Ilipokaribia saa sita za usiku, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kum sifu Mungu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. 26 Gha fla pakatokea tetemeko kubwa la nchi, hata msingi wa jengo la gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikawa wazi na mikatale yao ikafunguka. 27 Askari wa gereza alipoona kuwa milango ya gereza ni wazi, alivuta upanga wake ili ajiue, akidhani ya kuwa wafungwa wote wametoroka. 28 Lakini Paulo akapiga kelele kum zuia, akasema, “Usijidhuru kwa maana hatujatoroka, wote tuko hapa.” 29 Askari akaitisha taa iletwe, akaingia ndani ya chumba cha gereza, akapiga magoti akitetemeka miguuni mwa Paulo na Sila. 30 Kisha akawatoa nje akasema, “Ndugu zangu, nifanye nini ili nipate kuokoka?” 31 Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka, wewe pamoja na jamaa yako.” 32 Wakawaambia neno la Bwana yeye pamoja na wote waliokuwa wanaishi nyumbani kwake. 33 Yule askari akawachukua saa ile ile akaosha majeraha yao, naye akabatizwa pamoja na wote waliokuwa nyumbani kwake. 34 Aka wachukua, akawaandalia chakula nyumbani kwake, naye akafurahi pamoja na jamaa yake kwa kuwa alikuwa amemwamini Mungu.

Read full chapter