28 Kwa maana Roho Mtakatifu ameona vyema na sisi tume kubaliana tusiwatwike mzigo mkubwa zaidi ya mambo yafuatayo ambayo ni ya lazima: 29 kwamba msile cho chote kilichotolewa sadaka katika ibada za sanamu, kunywa damu, nyama ya wanyama wal ionyongwa; na muepukane na uasherati. Mkijitenga na mambo haya mtakuwa mmefanya vyema. Kwaherini.”

30 Wale wajumbe walipokwisha kuagwa, wakaondoka wakaenda Antiokia, wakakusanya ushirika wote wa waamini, wakawapa ile barua.

Read full chapter