Mahubiri ya Injili huko Ikonio

14 Basi huko Ikonio Paulo na Barnaba waliingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi. Wakahubiri kwa uwezo mkuu na umati mkubwa wa watu wakaamini, Wayahudi pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini wale Wayahudi ambao hawakupokea neno la Mungu, waliwa chochea watu wa mataifa dhidi ya wale walioamini. Paulo na Bar naba wakakaa huko kwa muda mrefu wakifundisha kwa ujasiri juu ya Bwana, ambaye alithibitisha kuwa mahubiri yao yalikuwa ni neno la neema yake; akawapa uwezo wa kutenda ishara na maajabu.

Read full chapter