Add parallel Print Page Options

11 Kanisa lote na watu wote waliosikia kuhusu hili waliingiwa hofu.

Uthibitisho kutoka kwa Mungu

12 Mitume walipewa nguvu ya kufanya ishara nyingi za miujiza na maajabu katikati ya watu. Walikuwa wanakutanika pamoja mara kwa mara katika eneo la Hekalu lililoitwa Ukumbi wa Sulemani. 13 Hakuna mtu yeyote ambaye hakuwa mwamini alikaa na kushirikiana nao, lakini kila mtu alisema mambo mazuri juu yao.

Read full chapter