Add parallel Print Page Options

24 Waamini waliposikia hili, wote kwa pamoja wakamwomba Mungu wakiwa na nia moja. Wakasema, “Bwana wa wote, wewe ndiye uliyeumba mbingu, dunia, bahari na kila kitu ulimwenguni. 25 Baba yetu Daudi alikuwa mtumishi wako. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu aliandika maneno haya:

‘Kwa nini mataifa yanatenda kwa kiburi?
    Kwa nini watu wanapanga mipango isiyofaa kama hii?
26 Wafalme wa dunia hujiandaa kwa mapigano,
    na watawala hukusanyika pamoja kinyume na Bwana
    na kinyume na Masihi wake.’(A)

Read full chapter