22 Lakini tungependa kusi kia mawazo yako kwa sababu tunajua kwamba kila mahali watu wana zungumza mabaya kuhusu dhehebu hili.” 23 Basi wakapanga siku ya kumsikiliza, na ilipofika, wakaja watu wengi mahali alipokuwa anakaa Paulo. Akawaeleza kuhusu Ufalme wa Mungu tangu asubuhi hadi jioni, akijaribu kuwahakikishia juu ya Yesu akitumia Maan diko ya Musa na Manabii. 24 Baadhi yao wakakubali, wakaamini, lakini wengine wakakataa kuamini.

Read full chapter