Add parallel Print Page Options

15 Nina tumaini katika Mungu kama walilonalo Wayahudi hawa, kwamba watu wote, wema na wabaya, watafufuliwa kutoka kwa wafu. 16 Hii ndiyo sababu daima nimejaribu kufanya kile ninachoamini kuwa sahihi mbele za Mungu na kila mtu.

17-18 Nimekuwa mbali na Yerusalemu kwa miaka mingi. Nilikwenda kule nikiwa na fedha za kuwasaidia watu wangu. Pia nilikuwa na sadaka za kutoa Hekaluni. Nilipokuwa nafanya hivyo, baadhi ya Wayahudi waliponiona pale. Nilikuwa nimemaliza ibada ya utakaso.[a] Sikufanya vurugu yoyote, na hakuna watu waliokuwa wamekusanyika kunizunguka. Read full chapter

Footnotes

  1. 24:17-18 ibada ya utakaso Vitu muhimu ambavyo Wayahudi walifanya ili kuikamilisha nadhiri ya mnadhiri. Tazama Mnadhiri katika Orodha ya Maneno.