Add parallel Print Page Options

28 Imempendeza Roho Mtakatifu na sisi kwamba tusiwatwishe mizigo ya ziada, isipokuwa kwa mambo haya ya muhimu:

29 Msile chakula kilichotolewa kwa sanamu.

Msile nyama inayotokana na wanyama walionyongwa au nyama ambayo bado ina damu ndani yake.

Msijihusishe na uzinzi.

Mkijitenga na mambo haya, mtakuwa mnaenenda vyema.

Wasalamu.

30 Hivyo Paulo, Barnaba, Yuda, na Sila waliondoka Yerusalemu na kwenda Antiokia. Walipofika huko walilikusanya kundi la waamini pamoja na wakawapa barua.

Read full chapter