Yesu Amponya Mtu Aliyepooza

Yesu akaingia katika mashua akavuka ziwa, akafika katika mji wa kwao. Watu wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye kitanda chake. Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mtu ali yepooza, “Mwanangu, jipe moyo; dhambi zako zimesamehewa.” Baadhi ya walimu wa sheria wakawaza moyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” Lakini Yesu alifahamu mawazo yao. Akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? Kwani ni lipi lililo rahisi: kusema ‘Dhambi zako zimesamehewa Lakini, nitawathibitishia kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Akamwambia yule aliyepo oza, “Simama, chukua kitanda chako uende nyumbani.” Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani. Watu walipoyaona haya, wakaogopa, wakamtukuza Mungu ambaye alitoa uwezo wa jinsi hii kwa wanadamu.

Yesu Amwita Mathayo

Yesu alipoondoka hapo, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi katika ofisi ya kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate”. Mathayo akainuka, akamfuata. 10 Wakati Yesu alipo kuwa ameketi mezani kula chakula katika nyumba fulani, watoza kodi wengi na wenye dhambi walikuja kula pamoja naye na wanafunzi wake. 11 Mafarisayo walipoona mambo haya wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini mwalimu wenu anakula na watoza kodi na wenye dhambi?” 12 Lakini Yesu alipowasikia aliwaambia, “ Watu wenye afya hawahitaji daktari, lakini wagonjwa wanamhitaji. 13 Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya, ‘Napenda huruma na wala sio sadaka za kuteketeza.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”

Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga

14 Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walikuja kwa Yesu wakamwuli za, “Mbona sisi na Mafarisayo tunafunga lakini wanafunzi wako hawafungi?” 15 Yesu akawajibu, “Hivi inawezekana wageni wali oalikwa harusini kuomboleza wakati bwana harusi yuko nao? Wakati utafika ambapo bwana harusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo wataka pofunga. 16 Hakuna mtu anayeweka kiraka kipya kwenye nguo kuu kuu, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye nguo hiyo na tundu litakalotokea litakuwa kubwa zaidi ya lile la mwanzo. 17 Wala watu hawahifadhi divai mpya kwenye viriba vikuukuu; wakifanya hivyo, viriba vitapasuka na divai itamwagika. Lakini divai mpya huwekwa katika viriba vipya na kwa njia hiyo divai na viriba husalimika.”

Yesu Amponya Mwanamke Aliyetokwa Damu

18 Wakati Yesu akiwa anawaambia haya, akaja afisa fulani akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amefariki lakini tafadhali uje umwekee mkono wako juu yake naye atakuwa hai.” 19 Yesu akasimama akamfuata. Wanafunzi wake pia wakaan damana naye.

20 Akatokea mwanamke mmoja ambaye alikuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu akagusa upindo wa nguo yake, 21 kwa maana alisema moyoni mwake, “Nikigusa tu nguo yake, nitaponywa.” 22 Yesu akageuka, na alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo, imani yako imekuponya.” Na wakati huo huo yule mwanamke akapona.

Yesu Amfufua Binti Wa Afisa

23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule afisa, aliwakuta waom bolezaji wanapiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele. 24 Akawaambia, “Ondokeni! Kwa maana binti huyu hakufa, bali amelala.” Wakamcheka kwa dhihaka. 25 Lakini watu walipok wisha tolewa nje, aliingia ndani akamshika mkono yule binti, naye akaamka. 26 Habari hizi zikaenea wilaya ile yote.

Yesu Aponya Vipofu

27 Yesu alipoondoka pale, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele kwa nguvu, “Mwana wa Daudi, tuhurumie.” 28 Alipoingia ndani wale vipofu walimfuata. Akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kuwafanya muone?” Wakamjibu, “Ndio Bwana.” 29 Ndipo Yesu akagusa macho yao akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyo amini.” 30 Macho yao yakafunguka. Naye akawaonya, “Angalieni mtu ye yote asijue jambo hili.” 31 Lakini wao walipoondoka walieneza sifa zake katika ile wilaya yote.

Yesu Amponya Bubu

32 Walipokuwa wakiondoka, watu walimletea mtu bubu, ali yekuwa amepagawa na pepo. 33 Na yule pepo alipofukuzwa, yule aliyekuwa bubu aliweza kusema. Ule umati wa watu wakastaajabu, wakasema, “Jambo kama hili halijawahi kuonekana katika Israeli.” 34 Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo kwa uwezo wa mkuu wa pepo.”

Wafanyakazi Ni Wachache

35 Yesu akazunguka kwenye miji yote na vijiji vyote akifundi sha katika masinagogi na kuhubiri Habari Njema za Ufalme, na kuponya kila ugonjwa na kila udhaifu. 36 Alipoona umati wa watu, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanateseka pasipo msaada, kama kondoo wasio na mchungaji.

37 Akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini wafa nyakazi ni wachache; 38 basi mwombeni Bwana wa mavuno ili awape leke wafanyakazi kwenye mavuno yake.”