Matayo 3
Neno: Bibilia Takatifu
Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji
3 Siku hizo Yohana Mbatizaji alitokea akihubiri katika nyika ya Yudea, akisema, 2 “Tubuni, muache dhambi zenu, mumgeukie Mungu; kwa maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.” 3 Huyu ndiye aliyezungumzwa na nabii Isaya aliposema, “Sauti ya mtu anayeita kwa sauti kubwa huko nyikani, ‘Tayarisheni njia ya Bwana, nyoosheni sehemu zote atakazopitia.’ ”
4 Yohana Mbatizaji alivaa nguo zilizotengenezwa kwa manyoya ya ngamia na kiunoni mwake alijifunga mkanda wa ngozi; chakula chake kilikuwa nzige na asali mwitu. 5 Watu walimwendea kutoka Yerusalemu, Yudea yote na bonde lote la mto Yordani. 6 Nao walipoungama dhambi zao aliwabatiza katika mto Yordani. 7 Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili awabatize, aliwaambia, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya muepuke ghadhabu inayokuja? 8 Basi thibitisheni kwa mwenendo mwema kwamba mmeziacha dhambi zenu. 9 Wala msidhani mnaweza kujitetea mkisema, ‘Sisi ni wana wa Ibrahimu 10 Na hata sasa shoka la hukumu ya Mungu limewekwa tayari katika mashina ya miti. Kila mti usiozaa matunda mazuri, utakatwa katwa na kutupwa motoni.
11 “Mimi nawabatiza kwa maji kama ishara kwamba mmetubu dhambi zenu. Lakini baada yangu anakuja aliye mkuu kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuchukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Pepeto lake liko mkononi, naye atasafisha pa kupepetea nafaka, na ngano yake ataiweka ghalani; lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.”
Yesu Abatizwa
13 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yordani ili abatizwe na Yohana. 14 Yohana alitaka kumzuia akimwambia, “Mimi ndiye ninahitaji kubatizwa na wewe, mbona unakuja kwangu? ” 15 Lakini Yesu akamjibu, “Kubali iwe hivi kwa sasa; kwa maana inatupasa kutimiza haki yote.” Kwa hiyo Yohana akakubali.
16 Na Yesu alipokwisha kubatizwa alitoka kwenye maji, ghafla mbingu zilifunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua aka kaa juu yake. 17 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ndiye
Matthew 3
King James Version
3 In those days came John the Baptist, preaching in the wilderness of Judaea,
2 And saying, Repent ye: for the kingdom of heaven is at hand.
3 For this is he that was spoken of by the prophet Esaias, saying, The voice of one crying in the wilderness, Prepare ye the way of the Lord, make his paths straight.
4 And the same John had his raiment of camel's hair, and a leathern girdle about his loins; and his meat was locusts and wild honey.
5 Then went out to him Jerusalem, and all Judaea, and all the region round about Jordan,
6 And were baptized of him in Jordan, confessing their sins.
7 But when he saw many of the Pharisees and Sadducees come to his baptism, he said unto them, O generation of vipers, who hath warned you to flee from the wrath to come?
8 Bring forth therefore fruits meet for repentance:
9 And think not to say within yourselves, We have Abraham to our father: for I say unto you, that God is able of these stones to raise up children unto Abraham.
10 And now also the axe is laid unto the root of the trees: therefore every tree which bringeth not forth good fruit is hewn down, and cast into the fire.
11 I indeed baptize you with water unto repentance. but he that cometh after me is mightier than I, whose shoes I am not worthy to bear: he shall baptize you with the Holy Ghost, and with fire:
12 Whose fan is in his hand, and he will throughly purge his floor, and gather his wheat into the garner; but he will burn up the chaff with unquenchable fire.
13 Then cometh Jesus from Galilee to Jordan unto John, to be baptized of him.
14 But John forbad him, saying, I have need to be baptized of thee, and comest thou to me?
15 And Jesus answering said unto him, Suffer it to be so now: for thus it becometh us to fulfil all righteousness. Then he suffered him.
16 And Jesus, when he was baptized, went up straightway out of the water: and, lo, the heavens were opened unto him, and he saw the Spirit of God descending like a dove, and lighting upon him:
17 And lo a voice from heaven, saying, This is my beloved Son, in whom I am well pleased.
Copyright © 1989 by Biblica