Yesu Afufuka

28 Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ile ya Jumapili, Mari amu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikwenda kuliangalia kaburi. Ghafla pakatokea tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu Malaika wa Bwana alikuja kutoka mbinguni akalisogeza lile jiwe, akalikalia. Malaika huyo alifanana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. Wale walinzi wa kaburi walipomwona walitetemeka kwa hofu, wakawa kama wamekufa.

Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope. Ninajua kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. Hayupo hapa. Amefu fuka kama alivyosema. Njooni muone pale alipokuwa amelazwa. Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake hivi, amefufuka kutoka kwa wafu naye amewatangulia kwenda Galilaya, mtamwona huko. Sasa nimekwisha waambia.” Wakiwa wamejawa na hofu na furaha nyingi, wale wanawake waliondoka upesi pale kaburini, wakaenda mbio kuwaeleza wanafunzi habari hizo.

Mara, Yesu akawatokea, akawasalimia, “Salamu!” Wale wana wake wakamwendea wakajitupa chini wakaishika miguu yake, wakam wabudu. 10 Ndipo Yesu akawaambia, “Msiogope. Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, wataniona huko.”

Taarifa Ya Askari

11 Wakati wale wanawake walipokuwa wanakwenda, baadhi ya wale askari waliokuwa wanalinda kaburi, wakaenda mjini kuwaeleza makuhani wakuu yote yaliyotokea. 12 Baada ya kufanya mkutano na wazee na kushauriana, waliwapa wale askari kiasi fulani cha fedha na 13 kuwaambia, “Semeni, ‘Wanafunzi wake walikuja wakamwiba usiku sisi tukiwa tumelala.’ 14 Kama habari hizi zikimfikia gavana, sisi tutamridhisha na hamtapata shida yo yote.” 15 Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha wakafanya kama walivy oagizwa. Na habari hii imeenea kwa Wayahudi mpaka leo.

Yesu Awatuma Wanafunzi Wake

16 Basi wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya kwe nye ule mlima ambao Yesu aliwaagiza. 17 Walipomwona, walimwabu du. Lakini baadhi yao waliona mashaka.

18 Yesu akawakaribia akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Kwa hiyo nendeni mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu: mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.