Yesu Afufuka

28 Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ile ya Jumapili, Mari amu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikwenda kuliangalia kaburi. Ghafla pakatokea tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu Malaika wa Bwana alikuja kutoka mbinguni akalisogeza lile jiwe, akalikalia. Malaika huyo alifanana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. Wale walinzi wa kaburi walipomwona walitetemeka kwa hofu, wakawa kama wamekufa.

Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope. Ninajua kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. Hayupo hapa. Amefu fuka kama alivyosema. Njooni muone pale alipokuwa amelazwa. Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake hivi, amefufuka kutoka kwa wafu naye amewatangulia kwenda Galilaya, mtamwona huko. Sasa nimekwisha waambia.”

Read full chapter