Ndipo yakatimia yale aliyonena nabii Yeremia kwamba, “Walichukua vile vipande thelathini vya fedha, thamani aliyopangiwa na wana wa Israeli, 10 wakanunulia shamba la mfinyanzi kama Bwana alivyon iagiza.”

Yesu Mbele Ya Pilato

11 Yesu akapelekwa mbele ya gavana naye akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Hayo umetamka wewe.”

Read full chapter