Font Size
Mathayo 27:46-50
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mathayo 27:46-50
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
46 Yapata saa tisa alasiri Yesu alilia kwa sauti kuu akisema, “Eloi, Eloi, lema sabakthani?” yaani “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha peke yangu?”(A)
47 Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hili wakasema, “Anamwita Eliya.”[a]
48 Mtu mmoja alikimbia haraka akaenda kuchukua sponji, akaijaza siki, akaifunga kwenye fimbo na akanyoosha fimbo ili kumpa Yesu sponji ili anywe siki. 49 Lakini wengine walisema, “Usimjali. Tunataka tuone ikiwa Eliya atakuja kumsaidia.”
50 Yesu akalia kwa sauti kuu tena, kisha akafa.[b]
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Copyright © 2017 by Bible League International