Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa

36 “Hakuna ajuaye siku wala saa, hata malaika mbinguni wala Mwana, isipokuwa Baba peke yake. 37 Kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa atakaporudi Mwana wa Adamu. 38 Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia kwenye safina. 39 Nao hawakujua ni nini kitatokea mpaka gharika ilipokuja ika wakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa nitakapokuja mimi Mwana wa Adamu.

40 “Watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa. 41 Wanawake wawili watakuwa wanatwanga; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa.

42 “Kwa hiyo kesheni, kwa maana hamjui ni siku gani ataka pokuja Bwana wenu.

43 “Lakini fahamuni kwamba, kama mwenye nyumba angalifahamu ni saa ngapi za usiku ambapo mwizi atakuja, angalikaa macho asiache nyumba yake ivunjwe. 44 Kwa hiyo ninyi pia lazima muwe tayari kwa maana mimi Mwana wa Adamu nitakuja saa ambayo hamnita zamii.”

Read full chapter