11 na watatokea manabii wengi wa uongo ambao watawapotosha watu. 12 Kwa sababu uovu utakuwa umeenea sana, upendo wa watu wengi utapoa. 13 Lakini mtu atakayesimama imara mpaka mwisho, ataoko lewa. 14 Na hii Habari Njema ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni pote, kama ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utafika.

15 “Mtakapoona lile ‘Chukizo la Uharibifu’ linalozungumzwa na nabii Danieli limesimama mahali Patakatifu - msomaji na aelewe - 16 basi wale walioko Yudea wakimbilie milimani. 17 Aliyeko juu ya nyumba asishuke kuchukua vitu vyake ndani. 18 Aliyeko sham bani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. 19 Ole wao wanawake watakaokuwa na mimba na watakaokuwa wakinyonyesha siku hizo! 20 Ombeni ili mtakapokuwa mnakimbia, isiwe ni kipindi cha baridi au siku ya sabato. 21 Kwa maana kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa na ambayo haitatokea tena. 22 Kama siku hizo zisingepunguzwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angesalimika, lakini kwa ajili ya wale walioteu liwa na Mungu, siku hizo zitapunguzwa. 23 Wakati huo mtu aki waambia, ‘Tazama! Kristo yuko hapa!’ au ‘Kristo yule pale!’ msi sadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo na manabii wa uongo na watafanya ishara za ajabu na miujiza mingi ili kuwadanganya, hata ikiwezekana, wateule wa Mungu.

Read full chapter