Matayo 18-20
Neno: Bibilia Takatifu
Aliye Mkuu Katika Ufalme Wa Mbinguni
18 Wakati huo, wanafunzi walimjia Yesu wakamwuliza, “Ni nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa mbinguni?” 2 Yesu akam wita mtoto mdogo akamsimamisha mbele yao. 3 Kisha akasema, “Nawa hakikishieni kwamba msipobadilika na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni. 4 Kwa hiyo mtu ye yote anayejinyenyekeza akawa kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa mbinguni.
5 “Na ye yote anayemkaribisha mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, ananikaribisha mimi. 6 Lakini kama mtu ye yote anamsabab isha mmojawapo wa hawa wadogo wanaoniamini atende dhambi, ingali kuwa nafuu kwake afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake akazam ishwe katika kilindi cha bahari. 7 Ole kwa ulimwengu, kwa sababu ya mambo yanayosababisha watu kutenda dhambi! Mambo hayo lazima yawepo, lakini ole wake mtu yule ambaye huyaleta. 8 Ikiwa mkono wako au mguu wako unakusababisha utende dhambi, ukate, uutupilie mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja au mguu mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na miguu miwili lakini ukatupwa katika moto wa milele. 9 Na kama jicho lako lina kusababisha utende dhambi ling’oe, ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa katika moto wa Jehena.
10 “Angalia usimdharau mmojawapo wa hawa wadogo, kwa maana nawaambieni, malaika wao mbinguni wanaonana daima na Baba yangu aliye mbinguni.” [ 11 Maana mimi Mwana wa Adamu nilikuja kuokoa kilichopotea.]
Mfano Wa Kondoo Aliyepotea
12 “Mnaonaje? Kama mtu ana kondoo mia moja na mmoja wao akapotea, hatawaacha wale tisini na tisa mlimani aende kumtafuta yule aliyepotea? 13 Na akisha mpata, nawaambia kweli, anafurahi zaidi kwa ajili ya huyo kondoo mmoja kuliko kwa wale tisini na tisa ambao hawakupotea. 14 Hali kadhalika, Baba yenu wa mbin guni hapendi hata mmojawapo wa hawa wadogo apotee.”
Ndugu Yako Akikukosea
15 “Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwambie kosa lake mkiwa ninyi wawili peke yenu. Akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako. 16 Kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili kusudi wawepo mashahidi wawili au watatu wa kuthi bitisha jambo hilo. 17 Akikataa kuwasikiliza, liambie kanisa. Kama akikataa kulisikiliza kanisa, basi mhesabu yeye kama ni mpa gani au mtoza ushuru.
18 “Nawaambieni kweli, lo lote mtakalokataza duniani lita kuwa limekatazwa mbinguni. Na lo lote mtakaloruhusu duniani litaruhusiwa mbinguni.
19 “Tena ninawaambia, ikiwa wawili kati yenu mtakubaliana hapa duniani kuhusu jambo lo lote mnaloomba, Baba yangu wa mbin guni atawatimizia. 20 Kwa maana wanapokutana watu wawili au watatu katika jina langu, hapo mimi nipo pamoja nao.”
Hakuna Mwisho Wa Kusamehe
21 Kisha Petro akaja kwa Yesu akamwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami niendelee kumsamehe? Hata mara saba?” 22 Yesu akamjibu, “Sikuambii mara saba, bali saba mara sabini.”
Mfano Wa Mdaiwa Asiyesamehe
23 “Kwa hiyo Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme aliyetaka kukamilisha hesabu zake za fedha na watumishi wake. 24 Alipoanza kukagua hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa na deni la mamilioni ya shilingi, aliletwa kwake. 25 Na kwa kuwa alikuwa hawezi kulipa deni hilo, bwana wake aliamuru kwamba auzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vyote alivyo navyo, ili zipatikane fedha za kulipa deni lake.
26 “Yule mtumishi akapiga magoti, akamsihi yule bwana akisema, ‘Naomba univumilie, nitakulipa deni lako lote.’ 27 Yule bwana akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwachilia.
28 “Lakini yule mtumishi alipotoka, alikutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha shilingi chache. Akamkamata, akam kaba koo akimwambia, ‘Nilipe deni langu!’
29 “Yule mtumishi mwenzake akapiga magoti akamsihi akisema, ‘Naomba univumilie, nitakulipa deni lako lote.’ 30 Lakini akaka taa. Badala yake akampeleka afungwe gerezani mpaka aweze kulipa hilo deni.
31 “Watumishi wenzake walipoona mambo haya, walisikitika sana. Wakamwendea bwana wao wakamweleza yote yaliyotokea.
32 “Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu, uliponisihi, nilikusamehe deni lako lote. 33 Je, hukupaswa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhuru mia?’ 34 Kwa hasira yule bwana akamkabidhi yule mtumishi kwa askari wa gereza mpaka atakapomaliza kulipa deni lote.
35 “Na hivi ndivyo Baba yangu wa mbinguni atakavyomfanyia kila mmoja wenu ambaye hatamsamehe ndugu yake kwa moyo.”
Yesu Afundisha Kuhusu Talaka
19 Yesu alipomaliza kusema maneno haya, aliondoka Galilaya akaenda sehemu za Yudea, ng’ambo ya mto Yordani. 2 Umati mkubwa wa watu walimfuata, naye akawaponya huko.
3 Baadhi ya Mafarisayo wakamjia wakamtega kwa kumwuliza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote ile?”
4 Akawajibu, “Hamjasoma kwamba aliyewaumba tangu mwanzo ali waumba mume na mke 5 akawaambia, ‘Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake na aambatane na mkewe; na hao wawili wata kuwa mwili mmoja’? 6 Kwa hiyo hawawi wawili tena, bali ni mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitengan ishe.”
7 Wakamwuliza, “Kwa nini basi Musa aliagiza kwamba mtu anaweza kumpa mkewe hati ya talaka na kumwacha?” 8 Yesu akawa jibu, “Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu mioyo yenu ni migumu. Lakini tangu mwanzo haikukusudiwa iwe hivyo. 9 Nami nawaambieni, mtu ye yote anayemwacha mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, akaoa mke mwingine, anazini.” [“Na mtu anayemwoa mwanamke aliyepewa talaka pia anazini.”]
10 Wanafunzi wake wakamwambia, “Kama hivi ndivyo hali ilivyo kati ya mume na mke, basi ni afadhali mtu asioe!” 11 Yesu akajibu, “Si kila mtu anaweza kupokea mafundisho haya isipokuwa wale ambao Mungu amewajalia. 12 Kwa maana wako watu wasioweza kuoa kwa sababu wamezaliwa na hali hiyo; na wengine wamefanywa hali hiyo na binadamu; na pia wako wengine ambao wameamua kutokuoa kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni. Awezaye kuli pokea fundisho hili na alipokee.”
Yesu Awabariki Watoto Wadogo
13 Kisha watoto wadogo wakaletwa kwa Yesu ili aweke mikono yake juu yao na awaombee. Lakini wanafunzi wake wakawakemea wali owaleta. 14 Yesu akawaambia, “Waacheni watoto waje kwangu, msiwazuie; kwa maana Ufalme wa mbinguni ni wa walio kama hawa. 15 Alipokwisha wawekea mikono akaondoka.
Mtu Tajiri
16 Mtu mmoja alikuja kwa Yesu akamwuliza, “Mwalimu, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?”
17 Yesu akamjibu, “Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema . Lakini kama unataka kuingia uzimani, tii amri.”
18 Yule mtu akamwuliza, “Amri zipi?” Yesu akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, 19 waheshimu baba yako na mama yako na umpende jirani yako kama nafsi yako.”
20 Yule kijana akasema, “Zote hizi nimezitii. Ninapungukiwa na nini zaidi?”
21 Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda kauze vitu vyote ulivyo navyo na fedha utakazopata uwape maskini, nawe utakuwa umejiwekea hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.” 22 Yule kijana aliposikia hayo aliondoka kwa masikitiko, kwa sababu alikuwa tajiri sana.
Hatari Za Utajiri
23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, “Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni. 24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.” 25 Wanafunzi wake waliposikia haya walishangaa sana, wakamwuliza, “Ni nani basi anaweza kuokoka?” 26 Lakini Yesu akawatazama akawaambia, “Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu kila kitu kinawezekana.” 27 Ndipo Petro aka mwambia, “Na sisi tulioacha kila kitu tukakufuata tutapata nini?”
28 Yesu akawajibu, “Ninawahakikishia kwamba, katika dunia mpya, wakati mimi Mwana wa Adamu nitakapoketi kwenye kiti changu cha utukufu cha enzi, ninyi mlionifuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu yale makabila kumi na mawili ya Israeli. 29 Na kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu zake au dada zake au baba au mama au watoto wake au mashamba kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na atarithi uzima wa milele. 30 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.”
Mfano Wa Wafanyakazi Katika Shamba La Mizabibu
20 “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mtu mwenye shamba la mizabibu aliyeondoka alfajiri kwenda kutafuta vibarua wa kufanya kazi shambani kwake. 2 Wakapatana kuwa atawalipa msha hara wa kutwa, yaani dinari moja, akawapeleka shambani.
3 “Mnamo saa tatu akaondoka tena akawakuta watu wengine wamesimama sokoni bila kazi. 4 Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu na nitawalipa haki yenu.’ Kwa hiyo wakaenda. 5 Mnamo saa sita na pia saa tisa alion doka tena akafanya hivyo hivyo. 6 Mnamo saa kumi na moja akaon doka tena akawakuta watu wengine bado wanazurura. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’ 7 Wakamjibu, ‘Ni kwa kuwa hakuna aliyetuajiri.’ Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la miza bibu.’
8 “Ilipofika jioni, yule mwenye shamba akamwita msimamizi wa vibarua akamwambia, ‘Waite wafanyakazi uwalipe ujira wao, ukian zia na wale walioajiriwa mwisho na kuishia na wale walioajiriwa kwanza.’ 9 Wale vibarua walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakaja na kila mmoja wao akalipwa dinari moja. 10 Basi wale wal ioajiriwa kwanza walipofika, walidhani watalipwa zaidi. Lakini kila mmoja wao pia alipewa dinari moja. 11 Walipoipokea, wakaanza kumlalamikia yule mwenye shamba wakisema, 12 ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu. Ime kuwaje wewe ukawalipa sawa na sisi ambao tumefanya kazi ngumu na kuchomwa na jua mchana kutwa?’
13 “Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sija kudhulumu. Je, hatukupatana kwamba utafanya kazi kwa dinari moja? 14 Chukua haki yako uende. Mimi nimeamua kumlipa huyu mtu ali yeajiriwa mwisho sawa na wewe. 15 Je, siwezi kufanya nipendavyo na mali yangu? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’ 16 Hali kadhalika, wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”
Yesu Azungumza Tena Kuhusu Kifo Chake
17 Yesu alipokuwa akienda Yerusalemu aliwachukua kando wale wanafunzi wake kumi na wawili akawaambia, 18 “Sasa tunakwenda Yerusalemu na mimi Mwana wa Adamu nitatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na walimu wa sheria nao watanihukumu adhabu ya kifo 19 na kunikabidhi kwa watu wa mataifa ambao watanizomea na kunipiga mijeledi na kunisulubisha; na siku ya tatu nitafufuliwa.”
Ombi La Mama Wa Wana Wa Zebedayo
20 Kisha mama yao wana wa Zebedayo akaja kwa Yesu akiwa na wanae, akapiga magoti akamwomba aseme neno.
21 Yesu akamwuliza, “Unataka nini?” Akajibu, “Tafadhali, ruhusu wanangu hawa, waketi mmoja upande wako wa kulia na mwin gine upande wako wa kushoto katika Ufalme wako.”
22 Yesu akawaambia, “Hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kuny wea kikombe nitakachonywea mimi?” Wakajibu, “Tunaweza.’ ’
23 Akawaambia, “Kikombe changu mtakinywea. Lakini kuhusu kuketi kulia au kushoto kwangu, sina mamlaka ya kuwaruhusu. Nafasi hizo ni za wale ambao Baba yangu amewaandalia.”
24 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya waliwakasi rikia hao ndugu wawili. 25 Lakini Yesu akawaita wote pamoja aka waambia, “Mnafahamu kuwa watawala wa mataifa hupenda kuheshi miwa, na wenye vyeo hupenda kuonyesha mamlaka yao. 26 Isiwe hivyo kwenu. Badala yake, anayetaka kuwa mkuu kati yenu hana budi kuwa mtumishi wenu. 27 Na anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu ni lazima awe mtumishi wenu; 28 kama vile ambavyo mimi Mwana wa Adamu sikuja ili nitumikiwe bali kutumika na kutoa maisha yangu kuwa fidia kwa ajili ya watu wengi.”
Yesu Awaponya Vipofu Wawili
29 Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu, walimfuata. 30 Vipofu wawili waliokuwa wameketi kando ya barabara waliposikia kwamba ni Yesu aliyekuwa akipita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuonee huruma.” 31 Watu wakawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao walizidi kupiga kelele wakisema, “ Bwana, Mwana wa Daudi, tuonee huruma.” 32 Yesu akasimama na akawaita, akawau liza, “Mnataka niwafanyie nini?” 33 Wakamjibu, “Bwana tuna taka kuona.”
34 Yesu akawaonea huruma, akawagusa, na mara wakaweza kuona; wakamfuata.
Copyright © 1989 by Biblica