Kisha Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri kwamba sisi tuko hapa. Ukiniruhusu, nitatengeneza vibanda vitatu hapa: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Eliya.”

Petro alipokuwa bado akizungumza, ghafla, wingu linalong’aa likatanda juu yao na sauti ikatoka kwenye wingu hilo ikasema, “Huyu ni mwanangu mpendwa, ambaye nimependezwa naye; msikilizeni yeye.” Wanafunzi waliposikia haya walianguka chini kifudifudi wakajawa na hofu.

Read full chapter