Maelezo Ya Mfano Wa Mbegu

18 “Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi aliyepanda mbegu. 19 Mtu anaposikia neno la Ufalme na asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake; hii ndio mbegu iliyopandwa njiani. 20 Mbegu iliyopandwa kwenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na kulipokea mara moja kwa furaha.

Read full chapter