Yesu Ni Bwana Wa Sabato

12 Wakati huo Yesu alipitia kwenye mashamba ya ngano siku ya sabato. Wanafunzi wake walikuwa na njaa, wakaanza kuvunja masuke ya ngano na kula. Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili wakam wambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanya siku ya sabato.”

Yesu akawajibu, “Hamjasoma walichofanya Daudi na wafuasi wake walipokuwa na njaa? Waliingia katika nyumba ya Mungu wakala mkate uliowekwa wakfu, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya isipokuwa makuhani peke yao. Au hamjasoma katika sheria kwamba siku ya sabato makuhani huvunja sheria ya sabato Hekaluni lakini hawahesabiwi kuwa na hatia? Nawaambieni wazi kwamba, aliye mkuu kuliko Hekalu yupo hapa. Na kama mngalifahamu maana ya maneno haya, ‘Ninataka rehema wala si sadaka ya kuteketezwa;’ msingeliwalaumu watu wasio na hatia, kwa maana Mwana wa Adamu ni Bwana wa sabato.”

Yesu Anamponya Mtu Aliyepooza Mkono

Yesu alipoondoka hapo, aliingia katika sinagogi lao. Huko alikuwepo mtu aliyepooza mkono . 10 Wakitafuta sababu ya kumsh taki, wakamwuliza, “Je, ni halali kuponya siku ya sabato?” 11 Yesu akawajibu, “Ni nani kati yenu ambaye kondoo wake aki tumbukia shimoni siku ya sabato hatamtoa? 12 Mtu ana thamani kubwa sana kuliko kondoo. Kwa hiyo ni halali kutenda mema siku ya sabato.”

13 Ndipo akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akau nyoosha, nao ukapona ukawa mzima kama ule mwingine. 14 Lakini Mafarisayo wakatoka nje wakashauriana jinsi ya kumwangamiza

Mtumishi Aliyechaguliwa Na Mungu

15 Lakini Yesu akiyafahamu mawazo yao, aliondoka mahali hapo. Na watu wengi walimfuata naye akawaponya wote. 16 Akawa kataza wasimtangaze. 17 Hii ilikuwa ili yatimie maneno aliyosema nabii Isaya: 18 “Mtazameni mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu ambaye moyo wangu unapendezwa naye. Nitaweka Roho yangu juu yake , naye atatangaza haki kwa watu wa mataifa. 19 Hatabishana wala hatapiga kelele, sauti yake haitasikika mitaani. 20 Hataponda unyasi uliochubuliwa wala hatazima mshumaa unaokaribia kuzima, mpaka atakapoifanya haki ipate ushindi; 21 na watu wa mataifa wataweka tumaini lao katika jina lake.”

Yesu Na Beelzebuli

22 Kisha wakamletea kipofu mmoja ambaye pia alikuwa bubu na amepagawa na pepo. Yesu akamponya akaweza kusema na kuona. 23 Watu wote wakashangaa wakaulizana, “Je, yawezekana huyu ndiye Mwana wa Daudi?” 24 Lakini Mafarisayo waliposikia haya wakasema, “Mtu huyu anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli, mfalme wa pepo wote.”

25 Yesu alifahamu mawazo yao, akawaambia, “Utawala wo wote ambao umegawanyika wenyewe kwa wenyewe utaanguka. Hali kadhalika mji wo wote au jamaa ye yote iliyogawanyika yenyewe kwa yenyewe haitadumu. 26 Na kama shetani anamfukuza shetani, atakuwa amega wanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utaendeleaje? 27 Na kama mimi hutoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, watu wenu je, wao hutoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao ndio watakaowaamulia. 28 Lakini kama ninatoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia. 29 Au inawezekanaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang’anya mali yake yote pasipo kwanza kumfunga yule mwenye nguvu? Akisha mfunga ndipo hakika anaweza kupora mali yake.

30 “Mtu asiyekuwa pamoja nami ananipinga; na mtu ambaye hakusanyi pamoja nami, anatawanya. 31 Kwa hiyo nawaambieni, watu watasamehewa kila aina ya dhambi na kufuru lakini mtu ata kayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.

32 “Na mtu atakayesema neno kumpinga Mwana wa Adamu ata samehewa, lakini ye yote atakayempinga Roho Mtakatifu hatasame hewa, katika ulimwengu huu wala katika ulimwengu ujao.”

Maneno Huonyesha Hali Ya Moyo

33 “Ili upate matunda mazuri lazima uwe na mti mzuri; ukiwa na mti mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulikana kwa matunda yake. 34 Ninyi uzao wa nyoka! Mnawe zaje kunena mema wakati ninyi ni waovu? Kwa maana mtu husema yaliyojaa moyoni mwake. 35 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutokana na hazina ya wema uliohifadhiwa ndani yake; na mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutokana na hazina ya uovu uliohifadhiwa ndani yake.

36 “Nawaambia hakika, siku ya hukumu watu watatakiwa kujieleza kuhusu kila neno lisilo la maana walilolisema. 37 Kwa maana kutokana na maneno yako utahesabiwa haki, na kutokana na maneno yako utahukumiwa.”

Ishara Ya Yona

38 Kisha baadhi ya waandishi wa sheria na Mafarisayo wakam wambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” 39 Lakini yeye akawajibu, “Kizazi cha watu waovu na wasiowaami nifu hutafuta ishara; lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokaa katika tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu nitakaa siku tatu, mchana na usiku ndani ya ardhi. 41 Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu wakati Yona alipowahubiria, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. 42 Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki; kwa kuwa yeye alisafiri kutoka miisho ya dunia ili akaisikilize hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.”

Mafundisho Kuhusu Pepo Mchafu

43 “Pepo mchafu akimtoka mtu, huzunguka sehemu kame akita futa mahali pa kupumzika, lakini hapati. 44 Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye ile nyumba yangu nilikotoka.’ Na anaporudi, anaikuta ile nyumba ikiwa tupu, imefagiliwa na kupangwa vizuri. 45 Kisha huenda na kuwaleta pepo wengine saba, wabaya zaidi kuliko yeye, nao huingia na kuishi huko. Na hali ya mwisho ya mtu huyo inakuwa mbaya zaidi kuliko mwanzo.”

Ndugu Wa Yesu

46 Wakati alipokuwa akizungumza na watu, mama yake na ndugu zake walisimama nje wakataka kuongea naye. [ 47 Mtu mmoja akam wambia, “Mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kuon gea na wewe.”] 48 Lakini akamjibu yule mtu aliyemwambia, “Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni nani?” 49 Akinyoosha kidole chake kwa wanafunzi wake, alisema , “Hawa hapa ndio mama yangu na ndugu zangu! 50 Kwa maana ye yote anayefanya mapenzi ya Baba yangu wa mbinguni, ndiye kaka, dada na mama yangu.”