Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili

10 Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa mamlaka ya kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Majina ya hao wanafunzi kumi na wawili ni haya: wa kwanza, Simon, ambaye aliitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo, mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; Filipo na Bartholomayo; Tomaso na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; Simoni Mkanaani; na Yuda Iskariote ambaye baadaye alimsaliti Yesu. Yesu aliwatuma hawa kumi na wawili, akawaagiza, “Msiende kwa watu wa mataifa wala msiingie mji wo wote wa Wasamaria. Bali waendeeni kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. Na mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia; Waponyeni wagonjwa, wafufueni wafu, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mmepo kea bure, toeni bure. Msichukue dhahabu, wala fedha wala sarafu za shaba katika mikanda yenu. 10 Msichukue mikoba ya safari, wala koti la pili, wala viatu, wala fimbo: kwa maana mfanyakazi anastahili riziki yake.

11 “Mkiingia katika mji au kijiji cho chote, mtafuteni mtu mwaminifu mkae kwake mpaka mtakapoondoka. 12 Kila nyumba mtakay oingia, toeni salamu. 13 Kama watu wa nyumba hiyo wanastahili, amani yenu na ikae kwao; na kama hawastahili, amani yenu itawaru dia ninyi. 14 Na kama mtu ye yote akikataa kuwapokea au kusiki liza maneno yenu, mtakapoondoka katika nyumba hiyo au mji huo, kung’uteni mavumbi yatakayokuwa miguuni mwenu. 15 Nawaambieni hakika, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Sodoma na Gomora kuliko itakavyokuwa kwa mji huo.”

Yesu Awatayarisha Wanafunzi Wake Kwa Mateso

16 “Ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo muwe werevu kama nyoka na wapole kama hua. 17 Jihadharini na watu, kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga viboko kwenye masinagogi yao. 18 Mtapelekwa mbele ya magavana na wafalme kwa ajili yangu mkatoe ushuhuda mbele yao na mbele ya watu wa mataifa. 19 Lakini mtakapokamatwa, msihangaike mkifiki ria mtakalosema; kwa maana mtaambiwa la kusema wakati huo. 20 Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkizungumza bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akisema kupitia kwenu. 21 Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanae auawe. Watoto nao wataasi wazazi wao na kusababisha wauawe. 22 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ataokoka. 23 Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kwa maana nawaambieni hakika, hamtamaliza kuipitia miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu hajafika.

24 “Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake wala mtumishi hamzidi bwana wake. 25 Inatosha ikiwa mwanafunzi atakuwa kama mwalimu wake na mtumishi kama bwana wake. Ikiwa wamethubutu kum wita bwana mwenye nyumba Beelzebuli, je, si watawasema vibaya zaidi jamaa ya mwenye nyumba?”

Anayestahili Kuogopwa

27 Ninalo waambia gizani, ninyi litamkeni mwangani: na lile mnalosikia likinong’onwa, litangazeni mkiwa mmesimama kwenye paa la nyumba. 28 Msiwaogope wale wawezao kuua mwili lakini hawawezi kuua roho; ila mwogopeni yeye ambaye anaweza kuiangamiza roho na mwili katika moto wa Jehena. 29 Mbayuwayu wawili huuzwa kwa sarafu moja tu. Lakini hata mmoja wao hawezi kuanguka pasipo Baba yenu kupenda. 30 Hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa. 31 Kwa hiyo msiogope; kwa maana ninyi mna thamani kubwa zaidi kuliko mbayuwayu wengi. 32 Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 33 Lakini ye yote atakayenikana mbele ya watu, mimi pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.”

Gharama Ya Kumfuata Yesu

34 “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali vita. 35 Kwa maana nimekuja kuleta kutokuele wana kati ya mtu na baba yake, na kati ya binti na mama yake, na kati ya mkwe na mama mkwe wake. 36 Na maadui wakubwa wa mtu watakuwa watu wa nyumbani kwake. 37 Ye yote anayempenda baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Na ye yote ampendaye mwanae au binti yake kuliko anavyoni penda mimi, hastahili kuwa wangu. 38 Na ye yote asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu. 39 Ata kayeng’ang’ania nafsi yake ataipoteza lakini aipotezae nafsi yake kwa ajili yangu ataipata.”

Watakaopokea Tuzo

40 “Mtu ye yote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi; na ye yote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye ali yenituma. 41 Mtu anayemkaribisha nabii kwa kuwa ni nabii, atapo kea tuzo ya nabii; na mtu anayemkaribisha mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapokea tuzo ya mwenye haki. 42 Na mtu ata kayetoa japo kikombe cha maji kwa mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, basi ninawaambieni hakika, hatakosa tuzo yake.”