19 Kwa kuwa Yosefu alikuwa mtu mwema hakutaka kumwaibisha mchumba wake Maria hadharani. Kwa hiyo aliamua kuvunja uchumba wao kwa siri. 20 Lakini alipokuwa bado anawaza juu ya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto akasema, “Yosefu mwana wa Daudi, usisite kumwoa Maria mchumba wako kwa maana mimba aliyo nayo ameipata kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atamzaa mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yesu; kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.”

Read full chapter