15 Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya mkutano pamoja na wazee na walimu wa sheria, na Baraza zima likafanya mashauri. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. Pilato akamwuliza, “Wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe ndiye uliyesema maneno hayo.” Makuhani wakuu wakamsh taki kwa mambo mengi. Pilato akamwuliza tena, “Huna la kujibu?

Unasikia mashtaka yao!”

Yesu hakusema neno. Pilato akashangaa.

Yesu Ahukumiwa Kifo

Ilikuwa desturi wakati wa sherehe za Pasaka kumfungulia mfungwa ye yote ambaye watu walimtaka . Wakati huo, mtu mmoja aitwaye Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na wahalifu wen gine kwa makosa ya kusababisha uasi ambapo mauaji yalitokea. Basi watu waliokusanyika walimjia Pilato wakamwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi wakati wa Pasaka. Pilato akawauliza, “Mnataka nimfungue huyu mfalme wa Wayahudi?” 10 Alikuwa ana fahamu kwamba wakuu wa makuhani walikuwa wanamwonea Yesu wivu ndio sababu wakamshtaki kwake. 11 Lakini makuhani wakuu wakawa chochea watu wamwombe awafungulie Baraba.

12 Pilato akawauliza tena watu, “Nimfanye nini huyu mtu mnayemwita mfalme wa Wayahudi?” 13 Wakapiga kelele, “Msulub ishe!” 14 Akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, “Msulubishe!”

15 Pilato alitaka kuwaridhisha watu, kwa hiyo akamfungulia Baraba; na baada ya kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa asulub ishwe.

Maaskari Wamdhihaki Yesu

16 Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17 Wakamvika Yesu vazi la zambarau, wakatengeneza taji ya miiba, wakamvika. 18 Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi!” 19 Wakampiga kwa fimbo kichwani, wakamte mea mate. Wakamdhihaki kwa kupiga magoti kama vile wanamheshimu mfalme. 20 Walipokwisha kumdhihaki, walimvua lile vazi la zam barau, wakamvika nguo zake. Kisha wakamtoa nje wakamsulubishe.

Yesu Asulubishwa

21 Walipokuwa wakienda kumsulubisha, njiani walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, raia wa Kirene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufas. Alikuwa anakuja mjini kutoka shamba. Wakamla zimisha abebe msalaba wa Yesu. 22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, -yaani Mahali pa Fuvu la Kichwa.

23 Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini akaikataa. 24 Basi wakamsulubisha, wakagawana nguo zake kwa kuzipigia kura kuamua kila mtu achukue nini.

25 Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 26 Tangazo la mashtaka yake liliandikwa maneno haya: “MFALME WA WAYAHUDI.” 27 Majambazi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wa kushoto. [ 28 Na kwa njia hii yale Maandiko yasemayo, “Alihesabiwa pamoja na wenye hatia,” yalitimia.] 29 Watu waliokuwa wakipita, walimtukana na kutikisa vichwa vyao kwa mzaha wakasema, “Si ulikuwa ukisema kwamba unaweza kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? 30 Shuka msalabani basi, ujiokoe mwenyewe!” 31 Hali kadhalika makuhani wakuu na walimu wa sheria walimdhihaki wakisema, “Ali waokoa wengine lakini anashindwa kujiokoa mwenyewe. 32 Kristo mfalme wa Wayahudi ashuke basi msalabani ili tupate kuona na kuamini!” Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia walimtukana.

Kifo Cha Yesu Msalabani

33 Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa tatu. 34 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi, Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” 35 Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu waliposikia maneno hayo, walisema, “Mnamsikia? Anamwita

Eliya!”

36 Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki, akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!”

37 Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kuanzia juu hadi chini.

39 Yule askari aliyekuwa amesimama mbele ya msalaba alipoona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”

40 Walikuwapo pia wanawake walio kuwa wakiangalia mambo haya kwa mbali. Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na pia Salome . 41 Hawa walifuatana na Yesu alipokuwa Galilaya na kumhudumia. Pia walikuwapo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja naye Yerusalemu.

Mazishi Ya Yesu

42 Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi, siku moja kabla ya Pasaka, 43 Yusufu wa Arimathea alijikaza akamwendea Pilato akamwomba auchukue mwili wa Yesu. Yeye alikuwa ni mjumbe wa Baraza aliyeheshimika, ambaye alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. 44 Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu amekwisha kufa. Kwa hiyo akamwita askari amhakikishie kuwa kweli amekufa. 45 Baada ya kuhakikishiwa na yule askari kwamba kweli amekufa, Pilato alimpa Yusufu ruhusa ya kuuchukua mwili wa Yesu. 46 Basi Yusufu alinunua sanda ya kitani, akautoa mwili wa Yesu msalabani; akamzungushia sanda, akamweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe akaufunika mlango wa kaburi. 47 Mariamu Magdalena na Mariamu mama wa Yose walipaona mahali alipozikwa Yesu.