Marko 14
Neno: Bibilia Takatifu
Mpango Wa Kumwua Yesu
14 Siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na sherehe ya mikate isiyotiwa chachu, makuhani wakuu na walimu wa sheria wali kuwa wakitafuta njia ya kumkamata Yesu kwa siri na kumwua. 2 Wakaambiana, “Jambo hili tusilifanye wakati wa sikukuu maana watu wanaweza kufanya ghasia.”
Yesu Apakwa Manukato
3 Yesu alikuwa Bethania nyumbani kwa Simoni ambaye aliwahi kuwa na ukoma. Alipokuwa mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia ndani akiwa na chupa ya alabasta yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu manukato hayo kichwani. 4 Baadhi ya watu waliokuwapo wali chukia wakasema, “Kwa nini anapoteza bure manukato hayo? 5 Si afadhali yangeliuzwa kwa dinari zaidi ya mia tatu na fedha hizo wakapewa maskini?” Wakamkemea huyo mama kwa hasira. 6 Lakini Yesu akawaambia, “Kwa nini mnamnyanyasa? Mwacheni! Amenitendea jambo zuri na jema. 7 Maskini mnao wakati wote na mnaweza kuwapa tia msaada wakati wo wote mtakapo. Lakini hamtakuwa nami wakati wote. 8 Huyu mama amenitendea lile aliloweza. Amenipaka manukato kuniandaa kwa mazishi yangu. 9 Nawaambieni hakika, mahali po pote duniani ambapo Habari Njema itahubiriwa, jambo hili alilo nitendea huyu mama, litatajwa kwa ukumbusho wake.”
Yuda Anapanga Kumsaliti Yesu
10 Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa makuhani wakuu kuwaambia kuwa yuko tayari kuwasaidia wamkamate Yesu. 11 Walifurahishwa sana na habari hizi, wakaahidi kumlipa fedha. Kwa hiyo yeye akaanza kutafuta nafasi nzuri ya kumsaliti.
Yesu Anakula Pasaka Na Wanafunzi Wake
12 Siku ya kwanza ya sherehe ya Mikate isiyotiwa chachu siku ambayo kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza Yesu, “Unapenda tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?” 13 Aka watuma wanafunzi wawili akawaagiza, “Nendeni mjini. Huko mtaku tana na mwanamume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni, 14 na pale atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, ‘Mwalimu anasema hivi, kiko wapi chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?’ 15 Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani kilichopangwa tayari. Tuandalieni humo.” 16 Wale wanafunzi walikwenda mjini wakakuta kila kitu kama alivyowaambia; wakaandaa chakula cha Pasaka. 17 Ilipofika jioni, Yesu akaja pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 18 Walipokuwa mezani wakila, akawaambia, “Ninawaam bia hakika, mmoja wenu anayekula pamoja nami, atanisaliti.” 19 Wote wakasikitika. Wakamwuliza mmoja mmoja, “Ni mimi, Bwana?” 20 Akawajibu, “Ni mmoja wenu kumi na wawili, yule anayechovya kipande chake cha mkate kwenye bakuli pamoja nami. 21 Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama maandiko yasemavyo. Lakini ole wake yeye atakayenisaliti. Ingelikuwa heri kama hakuz aliwa!”
Chakula Cha Bwana
22 Walipokuwa wakila, Yesu akachukua mkate, akashukuru , akaumega akawapa wanafunzi wake akisema, “Pokeeni, huu ni mwili wangu.” 23 Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa, wote wakanywa humo. 24 Akawaambia, “Hii ni damu yangu ya agano, inayomwagwa kwa faida ya wengi. 25 Nawaambieni hakika, sita kunywa tena divai mpaka siku ile nitakapokunywa divai mpya katika Ufalme wa Mungu.”
26 Walipokwisha kuimba wimbo walikwenda kwenye mlima wa
Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana
28 Yesu akawaambia, “Ninyi nyote mtakimbia mniache kwa maana imeandikwa: ‘Nitampiga mchungaji na kondoo watatawanyika.’ 29 Lakini nikisha fufuka nitawatangulia kwenda Galilaya. 30 Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.” Yesu akamwambia, “Ninakwambia hakika, usiku huu huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utakanusha mara tatu kwamba hunifahamu.” 31 Lakini Petro akasisitiza, “Hata kama ni lazima niuawe pamoja nawe, sitakukana.” Na wale wanafunzi wen gine wote wakasema hivyo hivyo.
Yesu Anasali Bustanini Gethsemane
32 Wakafika mahali paitwapo Gethsemane, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati mimi naomba.” 33 Kisha aka wachukua Petro na Yakobo na Yohana. Akawa na huzuni na uchungu mwingi. 34 Akawaambia, “Moyo wangu umejaa huzuni kiasi cha kufa; kaeni hapa mkeshe.” 35 Akaenda mbele kidogo, akajitupa chi ni akaomba kuwa kama ikiwezekana saa hiyo ya mateso aiepuke. 36 Akasema, “Aba, Baba, mambo yote yawezekana kwako. Tafadhali niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini si kama nitakavyo mimi, bali mapenzi yako yatimizwe.” 37 Akarudi, akakuta wame lala. Akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Hukuweza kukesha hata kwa saa moja? 38 Kesheni na kuomba msije mkaingia katika majar ibu. Roho i radhi lakini mwili ni dhaifu.” 39 Akaondoka tena akaenda kuomba akisema maneno yale yale. 40 Aliporudi tena ali wakuta wanafunzi wake wamelala; macho yao yalikuwa mazito na hawakujua la kumwambia. 41 Aliporudi mara ya tatu aliwaambia, “ Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imefika. Mimi Mwana wa Adamu ninatiwa mikononi mwa wenye dhambi. 42 Amkeni twendeni, tazameni, yule ambaye amenisaliti amekaribia.”
Yesu Akamatwa
43 Yesu alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akafika pamoja na umati wa watu wenye mapanga na marungu. Watu hao walikuwa wametumwa na makuhani wakuu, waandishi, na wazee. 44 Yuda, yule msaliti, alikuwa amewapa ishara wale watu kuwa, “Yule nitakayembusu, ndiye mnayemtaka, mkamateni na kumchukua akiwa chini ya ulinzi.”
45 Kwa hiyo Yuda alipofika, alimwendea Yesu akamwambia, “Mwalimu,” akambusu. 46 Wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi. 47 Lakini mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo aka chukua upanga akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. 48 Kisha Yesu akasema, “Mbona mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu? Kwani mimi ni jambazi? 49 Siku zote nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni wala hamkunikamata. Lakini Maandiko lazima yatimie. ” 50 Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia. 51 Kijana mmoja aliyekuwa amevaa shuka tu alikuwa akimfuata Yesu. Walipomkamata, 52 alikimbia uchi, akaacha shuka lake.
Yesu Afikishwa Barazani
53 Kisha wakampeleka Yesu nyumbani kwa kuhani mkuu ambapo makuhani wakuu, wazee, na walimu wa sheria walikuwa wamekuta nika. 54 Petro aliwafuata kwa mbali, akaingia barazani kwa kuhani mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto. 55 Makuhani wakuu na wajumbe wote wa Baraza walijaribu kutafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu ili wapate kumwua, lakini hawakupata. 56 Wengi walitoa ushahidi wa uongo, lakini ushahidi wao haukupatana.
57 Ndipo watu fulani wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo wakisema, 58 “Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitabomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga lin gine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ” 59 Lakini hata hawa, ushahidi wao ulipingana.
60 Kuhani Mkuu akasimama mbele ya Baraza akamwuliza Yesu, “Huwezi kujibu mashtaka haya ambayo watu hawa wameleta juu yako?” 61 Lakini Yesu alikaa kimya; hakusema neno lo lote. Kuhani Mkuu akamwuliza, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu Mtu kufu?” 62 Yesu akajibu, “Mimi ndiye, na mtaniona mimi Mwana wa Adamu nimeketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi, na nikija na mawingu ya mbinguni.”
63 Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi? 64 Ninyi wote mmemsikia akikufuru! Mna toa hukumu gani?” Wote wakamhukumu kwamba ana hatia na auawe.
65 Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa usoni wakampiga na kumwambia, “Toa unabii, utuambie nani amekupiga!” Maaskari wakampokea kwa mapigo.
Petro Amkana Yesu
66 Petro alikuwa bado yuko barazani. Kisha akaja mtumishi mmoja wa kike wa kuhani mkuu. 67 Alipomwona Petro akiota moto, alimtazama sana, akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 68 Lakini Petro akakataa, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema,” akaondoka akaenda mlangoni. 69 Yule mtumi shi wa kike akamwona, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama pale, “Huyu mtu ni mmoja wao.” 70 Lakini Petro akakana tena. Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja naye wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!” 71 Petro akaanza kulaani na kuapa, akawaambia, “Simjui huyo mtu mnayemsema.”
72 Hapo hapo jogoo akawika mara ya pili. Petro akakumbuka lile neno ambalo Yesu alikuwa amemwambia, “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akalia kwa uchungu. Pilato Anamhoji Yesu
马可福音 14
Chinese Contemporary Bible (Simplified)
谋害耶稣
14 再过两天就是逾越节和除酵节,祭司长和律法教师正暗暗地找机会拘捕、杀害耶稣。
2 他们说:“我们不能在节期那天下手,以免在百姓中引起骚乱。”
耶稣受膏
3 耶稣在伯大尼村患过麻风病的西门家里吃饭,有个女人带了一瓶极贵重的纯哪哒香膏进来,把玉瓶打破,将香膏倒在耶稣头上。 4 有些人生气地彼此议论说:“为什么这样浪费? 5 这瓶香膏可以卖三百多个银币[a]来周济穷人。”他们就责备那女人。
6 耶稣说:“随她吧!何必为难她呢?她在我身上做的是一件美事。 7 因为你们身边总会有穷人,你们随时都可以帮助他们,可是你们身边不会总有我。 8 她做了自己能做的。她是为我的安葬做准备,提前用香膏抹了我的身体。 9 我实在告诉你们,无论福音传到世界哪个角落,人们都会传扬这女人的事迹,纪念她。”
犹大出卖耶稣
10 十二门徒当中的加略人犹大去见祭司长,要把耶稣出卖给他们。 11 他们听了喜出望外,答应给他酬金。于是犹大伺机出卖耶稣。
最后的晚餐
12 除酵节的第一天,就是宰杀逾越节羔羊的那天,门徒问耶稣:“我们该到什么地方为你准备逾越节的晚餐呢?”
13 耶稣就派了两个门徒,并嘱咐他们:“你们进城会看到一个人带着一瓶水迎面而来,你们就跟着他。 14 他进哪一家,你们也跟着进去,对那家的主人说,‘我们的老师问你,祂的客房在哪里,祂要和门徒在里面吃逾越节的晚餐。’ 15 主人会带你们到楼上一间布置整齐的大房间,你们就在那里准备吧。”
16 两个门徒出去,进了城,所遇见的果然和耶稣所说的一样。他们预备了逾越节的晚餐。
17 傍晚时分,耶稣带着十二门徒来了。 18 用餐的时候,耶稣说:“我实在告诉你们,你们中间有一个人要出卖我,他现在正和我同桌吃饭。”
19 他们听了都感到不安,一个一个地问耶稣:“不是我吧?” 20 耶稣说:“是你们十二个人中的一个,他现在正和我一起在盘子里蘸饼吃。 21 人子一定会受害,正如圣经的记载,但出卖人子的人有祸了,他还不如不生在这世上!”
22 他们吃的时候,耶稣拿起饼来,祝谢后,便掰开,分给门徒,说:“拿去吃吧!这是我的身体。” 23 接着又拿起杯来,祝谢后,递给他们,他们都喝了。 24 耶稣说:“这是我为万人所流的立约之血。 25 我实在告诉你们,从今天起,一直到我在上帝的国喝新酒的那天之前,我不会再喝这葡萄酒。”
26 他们唱完诗歌,就出门去了橄榄山。
预言彼得不认主
27 耶稣对他们说:“你们都要背弃我,因为圣经上说,
“‘我要击打牧人,
羊群将四散。’
28 但我复活后,要先你们一步去加利利。”
29 彼得说:“即使所有人都背弃你,我也决不会背弃你!”
30 耶稣说:“我实在告诉你,就在今天晚上鸡叫两次以前,你会三次不认我。”
31 彼得郑重地说:“就算要我跟你一起死,我也不会不认你。”其他门徒也都这样说。
客西马尼园的祷告
32 他们到了客西马尼园,耶稣对门徒说:“你们坐在这里,我要去祷告。”
33 于是耶稣带着彼得、雅各和约翰向前走。祂觉得极其难过,非常伤痛, 34 说:“我心里非常忧伤,几乎要死,你们留在这里警醒。” 35 耶稣往前走了不远,俯伏在地祷告,如果可以,不要让那时刻临到祂。
36 祂说:“阿爸,父啊,你无所不能,求你撤去此杯。然而,愿你的旨意成就,而非我的意愿。”
37 祂回来,见他们都睡着了,就对彼得说:“西门,你在睡觉吗?你不能警醒一时吗? 38 你们要警醒祷告,免得陷入诱惑。你们的心灵虽然愿意,肉体却很软弱。”
39 耶稣又去祷告,所祈求的跟上次一样。 40 祂回来时见他们又睡着了,因为他们困得眼皮发沉,也不知道对祂说什么。 41 祂第三次祷告回来后,对他们说:“你们还在睡觉休息吗?够了,时候到了,看啊,人子要被出卖、交在罪人的手里了。 42 起来,我们走吧。看啊,出卖我的人已经来了!”
耶稣被捕
43 耶稣还在说话的时候,十二门徒之一的犹大已带了一群人拿着刀棍迎面而来。他们奉了祭司长、律法教师和长老之命来捉拿耶稣。 44 出卖耶稣的犹大预先和他们定了暗号,说:“我亲吻谁,谁就是耶稣,你们把祂抓起来,小心押走。”
45 犹大随即走到耶稣跟前说:“老师。”然后就亲吻耶稣。 46 其他人就下手捉拿耶稣。 47 站在旁边的一个门徒拔出刀朝大祭司的奴仆砍去,削掉了他一只耳朵。
48 耶稣问那群人:“你们像对付强盗一样拿着刀棍来抓我吗? 49 我天天和你们在一起,在圣殿里教导人,你们没有来抓我。你们现在这样做是要应验圣经的话。”
50 那时,门徒都撇下耶稣,各自逃命去了。 51 只有一个身上披着一块麻布的青年跟着耶稣。他们上去捉他, 52 他丢了那块麻布,赤身逃走了。
大祭司审问耶稣
53 他们把耶稣押到大祭司那里,众祭司长、长老和律法教师都来了。 54 那时彼得远远地跟着耶稣,一直来到大祭司的院子,与卫兵们坐在一起烤火。 55 祭司长和全公会的人正在寻找证据控告耶稣,要定祂死罪,只是找不到。 56 不少人作伪证控告祂,他们的证词却不一致。 57 后来,有几个人站起来作伪证说: 58 “我们听见祂说,‘我要拆毁这座人手建造的圣殿,三天内不靠人力另造一座。’” 59 即使这样,他们的证词也不一致。
60 最后,大祭司在众人面前站起来质问耶稣:“你不回答吗?这些人作证控告你的是什么呢?”
61 耶稣还是沉默不语,什么也不答。大祭司又问祂:“你是那当受称颂者的儿子基督吗?” 62 耶稣说:“我是!将来你们要看见人子坐在全能上帝的右边,驾着天上的云降临。”
63 大祭司便撕裂衣服,说:“我们还需要什么证人呢? 64 你们听见祂说亵渎的话了,你们看怎么办?”他们都判祂死罪。
65 有几个人向祂吐唾沫,蒙上祂的眼睛,挥拳打祂,嘲笑祂说:“你说预言吧!”卫兵押祂下去时,也打祂。
彼得三次不认耶稣
66 那时,彼得仍在院子里,大祭司的一个婢女走过来, 67 见彼得在烤火,打量了他一番,说:“你也是那个拿撒勒人耶稣的同伙。”
68 “我不知道也不明白你在说什么!”彼得一边否认,一边躲到外院去。那时,鸡叫了。
69 一会儿,那婢女又看见彼得,就对旁边的人说:“他是跟他们一伙的!” 70 彼得又加以否认。
再过了一会儿,旁观的人也指着彼得说:“你一定是跟他们一伙的,因为你也是加利利人!”
71 彼得又赌咒又发誓,说:“我根本不认识你们说的这个人。” 72 就在这时候,鸡又叫了。彼得突然想起耶稣曾对他说:“在鸡叫两次以前,你会三次不认我”,忍不住痛哭起来。
Footnotes
- 14:5 “三百多个银币”相当于当时人们一年的工钱。
Copyright © 1989 by Biblica
Chinese Contemporary Bible Copyright © 1979, 2005, 2007, 2011 by Biblica® Used by permission. All rights reserved worldwide.