Marko 10-12
Neno: Bibilia Takatifu
Yesu Afundisha Kuhusu Talaka
10 Yesu akaondoka mahali pale akavuka mto wa Yordani, akaenda sehemu ya Yudea. Umati wa watu ukamfuata tena na kama kawaida yake akawafundisha.
2 Baadhi ya Mafarisayo wakamjia wakitaka kumtega, wakamwul iza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake?”
3 Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuruje?” 4 Wakamjibu, “Musa aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.”
5 Yesu akawaambia, “Musa aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 6 Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mume na mke. 7 Na kwa sababu hii mume atamwacha baba yake na mama yake na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’ 8 Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja. 9 Basi, alichokiun ganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
10 Baadaye waliporudi nyumbani , wanafunzi wa Yesu walimwul iza kuhusu jambo hili.
11 Akawajibu, “Mtu ye yote anayempa mkewe talaka na kuoa mke mwingine, anazini kwa yule mke aliyempa talaka. 12 Na mwa namke anayempa mumewe talaka na kuolewa na mume mwingine, anazini pia.”
Yesu Anawabariki Watoto Wadogo
13 Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse lakini wanafunzi wake wakawakemea. 14 Yesu alipoona yaliyokuwa yakitokea alichukizwa, akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa watu kama hawa! 15 Ninawahakikishieni kwamba, mtu ye yote ambaye hataukubali Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.” 16 Akawakumbatia wale watoto wadogo, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.
Mtu Tajiri
17 Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini niurithi Ufalme wa milele?”
18 Yesu akamwambia, “Mbona unaniita mwema? Hakuna ali yemwema isipokuwa Mungu peke yake. 19 Unazifahamu amri ‘Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye. Waheshimu baba yako na mama yako .”’
20 Akamjibu, “Mwalimu, amri hizi zote nimezishika tangu nikiwa mtoto.”
21 Yesu akamtazama kwa moyo wa upendo akamwambia, “Umepun gukiwa na kitu kimoja tu. Nenda ukauze vitu vyote ulivyo navyo uwape maskini fedha utakazopata, nawe utakuwa na utajiri mbin guni; kisha njoo, unifuate.”
22 Yule mtu aliposikia hayo, alisikitika sana, akaondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa tajiri sana.
23 Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa
Mungu!”
24 Wanafunzi wake wakashtushwa sana na maneno hayo. Lakini Yesu akasema tena, “Wanangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalme wa Mungu. 25 Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”
26 Wanafunzi wake wakashangaa mno. Wakaulizana wao kwa wao, “Ni nani basi anaweza kuokolewa?”
27 Yesu akawatazama akawaambia, “Kwa wanadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu.” 28 Petro akaanza kumwambia, “Sisi tumeacha kila kitu tukakufu ata!”
29 Yesu akajibu, “Ninawaambieni hakika, hakuna mtu ye yote aliyeacha nyumba, kaka, dada, mama, baba, watoto au shamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya kuitangaza Habari Njema, 30 ambaye hatalipwa katika ulimwengu huu mara mia zaidi: nyumba, kaka, dada, mama, watoto, mashamba na mateso pia; na kupewa uzima wa milele katika ulimwengu ujao. 31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na wa mwisho watakuwa wa kwanza.”
Yesu Azungumzia Tena Kifo Chake
32 Walikuwa njiani kuelekea Yerusalemu na Yesu alikuwa ame tangulia. Wanafunzi wake walikuwa wamejawa na hofu, na watu wal iowafuata walikuwa wanaogopa. Yesu akawachukua tena wale wana funzi wake kumi na wawili kando akawaambia yatakayompata. 33 Akasema, “Tunakwenda Yerusalemu, na Mimi Mwana wa Adamu nitapelekwa kwa makuhani wakuu na walimu wa sheria; nao watanihu kumu adhabu ya kifo na kunikabidhi kwa mataifa. 34 Wao watanid hihaki na kunitemea mate na kunipiga na kuniua. Baada ya siku tatu, nitafufuka.”
Ombi La Yakobo Na Yohana
35 Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo wakamwendea Yesu wakamwambia, “Bwana, kuna jambo moja tungependa kukuomba.”
36 Akawauliza, “Mngependa niwafanyie jambo gani?”
37 Wakamjibu, “ Tunakuomba utakapoketi katika ufalme wako wa utukufu, uturuhusu tuketi pamoja nawe, mmoja wetu mkono wako wa kulia na mwingine mkono wako wa kushoto.”
38 Yesu akawaambia, “Hamjui mnaloliomba. Mko tayari kunywea kikombe cha mateso nitakachokunywa? Mnaweza kubatizwa ubatizo nitakaobatizwa?”
39 Wakamjibu, “ Tunaweza.” Yesu akawaambia, “Mtakunywa katika kikombe nitakachokunywa na kubatizwa ubatizo nitakaobati zwa. 40 Lakini kuhusu kuketi mkono wangu wa kulia au wa kushoto si juu yangu mimi kuwaruhusu. Mungu atatoa nafasi hizo kwa watu aliowaandalia.”
41 Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, waliwaka sirikia Yakobo na Yohana. 42 Yesu akawaita wanafunzi wake wote pamoja akawaambia, “Mnafahamu kwamba watu wanaotawala watu wa mataifa hutumia mabavu, na viongozi wa vyeo vya juu hupenda kuon yesha wana madaraka! 43 Lakini haipasi kuwa hivyo kati yenu. Badala yake, anayetaka kuwa mkuu kati yenu hana budi kuwa mtum ishi wenu, 44 na ye yote anayetaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa mtumishi wa wote. 45 Kwa maana hata mimi Mwana wa Adamu sikuja ili nitumikiwe, bali nilikuja ili niwe mtumishi na kutoa maisha yangu yawe fidia kwa ajili ya watu wengi.”
Yesu Amponya Kipofu Bartimayo
46 Wakafika Yeriko. Na Yesu alipokuwa akiondoka pamoja na Wanafunzi wake na umati wa watu, kipofu mmoja, jina lake Barti mayo, mwana wa Timayo, alikuwa ameketi kando kando ya njia, akiomba.
47 Aliposikia kuwa Yesu wa Nazareti alikuwa akipita, akaanza kupiga kelele, “Yesu, Mwana wa Daudi, nionee huruma!”
48 Watu wengi wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye alipiga kelele zaidi, “Mwana wa Daudi, nionee huruma!”
49 Yesu akasimama akawaambia, “Mwiteni.” Wakamwita wakamwambia, “Changamka! Usimame, anakuita.”
50 Akatupa vazi lake kando, akaruka juu, akamwendea Yesu. 51 Yesu akamwuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Yule kipofu akajibu, “Mwalimu, nataka kuona tena.” 52 Yesu akamwambia, “Nenda, imani yako imekuponya.” Wakati huo huo akaweza kuona, akamfuata Yesu njiani.
Yesu Aingia Yerusalemu
11 Walipokaribia Yerusalemu, wakiwa katika miji ya Bethfage na Bethania katika mlima wa Mizeituni, Yesu aliwatuma wanafunzi wake wawili watangulie. 2 Akawaagiza, “Nendeni kwenye kijiji kile kilichoko mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtam wona mwana punda amefungwa, ambaye hajawahi kupandwa na mtu ye yote. Mfungueni mumlete hapa. 3 Kama mtu atawauliza, ‘Mbona mnam fungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji na atamrudisha mara moja.’ ” 4-5 Wakaenda, wakamkuta mwana punda mmoja kando ya barabara, akiwa amefungwa kwenye mlango wa nyumba. Walipokuwa wakimfungua, watu waliokuwa wamesimama karibu wakauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwanapunda?” 6 Wakawajibu kama Yesu alivyokuwa amewaagiza, na wale watu wakawaruhusu.
7 Wakamleta huyo mwana punda kwa Yesu wakamtandikia mavazi yao, akaketi juu yake. 8-10 Watu wengi wakatandaza nguo zao barabarani na wengine wakatandaza matawi waliyokata mashambani. Na wote waliotangulia na wale waliofuata wakapaza sauti zao wakasema: “Hosana! Mungu apewe sifa! Mungu ambariki yeye anayekuja kwa jina la Bwana! Ubarikiwe Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi! Mungu asifiwe!”
11 Yesu akaingia Yerusalemu, akaenda Hekaluni akaangalia kila kitu. Lakini kwa kuwa ilikuwa jioni, akaenda Bethania na wale wanafunzi kumi na wawili.
Yesu Alaani Mtini Usiozaa
12 Kesho yake walipokuwa wanaondoka Bethania, Yesu alikuwa na njaa. 13 Alipouona mtini kwa mbali, alikwenda kuangalia kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, alikuta una majani tu kwa kuwa hayakuwa majira ya tini. 14 Yesu akauambia ule mti, “Hakuna mtu atakayekula tini kutoka kwako tena.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.
Yesu Afukuza Wafanya Biashara Hekaluni
15 Walipofika Yerusalemu, Yesu aliingia Hekaluni akaanza kuwafukuza watu waliokuwa wakifanya biashara humo. Akapindua meza za waliokuwa wakibadilisha fedha na viti vya watu waliokuwa wakiuza njiwa. 16 Hakuruhusu mtu ye yote kuchukua bidhaa kupi tia ukumbi wa Hekalu. 17 Akawafundisha akisema, “Je, haikuan dikwa katika Maandiko kuwa: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa watu wote’? Mbona ninyi mmeigeuza kuwa pango la wany ang’anyi?”
18 Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakapata habari. Wakatafuta njia ya kumwangamiza. Walimwogopa kwa sababu watu wal ikuwa wamevutiwa sana na mafundisho yake.
19 Ilipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake walikwenda nje ya mji.
Fundisho Kuhusu Ule Mtini Uliolaaniwa
20 Asubuhi yake walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini ume nyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. 21 Petro alikumbuka, akamwambia Yesu, “Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani umeny auka!”
22 Yesu akamjibu, “Mwamini Mungu. 23 Nawaambieni hakika, mtu akiuambia mlima huu, ‘Ondoka hapo nenda kajitupe baharini,’ akiamini pasipo kuwa na mashaka yo yote kwamba anayosema yata tendeka, atatimiziwa maombi yake. 24 Kwa hiyo nawaambieni, lo lote mnaloomba katika sala, aminini kwamba mmekwisha kulipokea nanyi mtapewa. 25 Nanyi mnaposimama kusali, sameheni kila mtu aliyewakosea ili Baba yenu wa mbinguni apate kuwasamehe ninyi makosa yenu.” [ 26 Lakini msipowasamehe wengine, basi makosa mliyofanya ninyi hayatasamehewa na Baba yenu wa mbinguni.]
Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake
27 Wakafika tena Yerusalemu. Wakati Yesu alipokuwa akitem bea Hekaluni, makuhani wakuu, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia 28 wakamwuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?
Na ni nani aliyekupa mamlaka hayo?”
29 Yesu akawajibu, “Nitawauliza swali mmoja. Mkinijibu, mimi pia nitawaeleza ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 30 Niambieni, mamlaka aliyotumia Yohana kubatiza watu, yalitoka kwa Mungu au kwa watu?”
31 Wakaanza kubishana, “Tukisema, ‘Yalitoka kwa Mungu’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 32 Je, tunaweza kusema ‘Yali toka kwa watu’? - Waliogopa watu kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa nabii. 33 Kwa hiyo wakamjibu, “Hatujui.” Na Yesu akawaambia, “Mimi pia sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”
Mfano Wa Shamba La Mizabibu Na Wakulima Waovu
12 Yesu alianza kusema nao kwa kutumia mifano: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akalizungushia uzio, akachimba kisima cha kutengenezea divai na akajenga mnara. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima fulani kisha akasafiri kwenda nchi nyingine. 2 Wakati wa mavuno ulipofika, mwenye shamba alimtuma mtumishi wake kwa hao wakulima kuchukua sehemu yake ya mavuno. 3 Lakini wale wakulima walimkamata yule mtumishi, wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. 4 Yule mwenye shamba akamtuma mtum ishi mwingine. Wale wakulima wakampiga kichwani, na kumfanyia mambo ya aibu. 5 Akapeleka mtumishi mwingine tena. Huyu, wakam wua. Akapeleka wengine zaidi, baadhi yao wakawapiga na wengine wakawaua. 6 Mwenye shamba akawa amebakiwa na mtu mmoja tu ambaye angeweza kumtuma. Huyu alikuwa mwanae aliyempenda sana. Hatimaye akaamua kumtuma akisema, ‘Bila shaka watamheshimu mwanangu.’ 7 Lakini wale wakulima wakashauriana, ‘Huyu mwanae ndiye mrithi. Tumwue na urithi utakuwa wetu.’ 8 Wakamchukua, wakamwua, wakam tupa nje ya shamba. 9 Mnadhani yule mwenye shamba atafanya nini? Atakuja, awaue hao wakulima kisha alikodishe shamba lake kwa wak ulima wengine. 10 Hamjasoma Maandiko haya? ‘Lile jiwe waliloli kataa wajenzi limekuwa jiwe kuu la msingi. 11 Jambo hili limefa nywa na Bwana, nalo ni la ajabu kwetu.’ ”
12 Viongozi wa Wayahudi wakatafuta njia ya kumkamata Yesu kwa sababu walifahamu kuwa mfano huo uliwasema wao. Lakini wali waogopa watu. Kwa hiyo walimwacha wakaondoka, wakaenda zao. Kuhusu Kulipa Kodi
13 Mafarisayo kadhaa na Maherode walitumwa kuja kumtega Yesu katika maneno yake. 14 Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunafahamu kuwa wewe huwaambia watu ukweli pasipo kujali watu watasema nini. Wala hujali cheo cha mtu bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. Je, ni halali au si halali kulipa kodi kwa Kais ari? 15 Tulipe kodi hiyo au tusilipe?” Lakini Yesu alitambua hila yao. Akawaambia, “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni sar afu niione.” 16 Wakamletea. Akawauliza, “Hii ni picha ya nani na hii ni sahihi ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.”
17 Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vilivyo vya Kais ari na vya Mungu mpeni Mungu.” Jibu hili liliwastaajabisha sana.
Kuhusu Ufufuo wa Wafu
18 Kisha Masadukayo, ambao wanaamini kuwa hakuna ufufuo wa wafu, walimjia Yesu wakamwuliza swali wakisema, 19 “Mwalimu, Musa alituandikia agizo kuwa kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila mtoto, basi ndugu yake hana budi kumwoa mjane huyo ili amzalie ndugu yake watoto. 20 Sasa walikuwapo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa akafariki pasipo kupata mtoto. 21 Wapili akam woa yule mjane, naye akafariki bila kuacha mtoto. Ikawa hivyo hata kwa yule wa tatu. 22 Kwa kifupi, ndugu wote saba walimwoa huyo mjane lakini wote hawakuzaa naye. Hatimaye yule mama naye akafariki. 23 Sasa tuambie, wakati wa ufufuo, watakapofufuka wote, huyo mama aliyeolewa na ndugu wote saba, atakuwa mke wa nani?”
24 Yesu akawajibu, “Mmekosea kabisa kwa maana hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu.” 25 Wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni . 26 Na kuhusu ufufuo wa wafu: hamjasoma katika kitabu cha Musa, sehemu ile inayoelezea jinsi Mungu alivyozungumza na Musa kutoka katika kichaka akisema, ‘Mimi, ni Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? 27 Mungu si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai. Kwa hiyo mmekosea kabisa.”
Amri Iliyo Kuu
28 Mwalimu mmoja wa sheria aliwasikiliza wakijadiliana. Alipoona kwamba Yesu amewajibu vizuri, naye akamwuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?” 29 Yesu akamjibu, “Iliyo kuu ni hii, ‘Sikiliza Israeli, Bwana Mungu wetu ndiye Bwana pekee. 30 Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’ 31 Na sheria ya pili kwa ukuu ndio hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”
32 Yule mwalimu wa sheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, ume jibu vyema. Ulivyosema ni kweli kabisa, Mungu ni mmoja wala hakuna mwingine ila yeye. 33 Na kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote; na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka ya kuteketezwa.”
34 Yesu alipoona jinsi alivyojibu kwa busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.” Tangu wakati huo, hakuna mtu aliyethubutu kumwuliza maswali zaidi.
Kuhusu Mwana Wa Daudi
35 Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, aliuliza, “Mbona walimu wa sheria wanasema kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi? 36 Kwa maana Daudi akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema, ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: keti mkono wangu wa kulia mpaka niwashi nde na kuwafedhehesha maadui zako chini ya miguu yako.’ 37 Ikiwa Daudi mwenyewe anamwita Bwana, yawezekanaje tena Kristo akawa mwanawe?” Watu wote wakamsikiliza kwa furaha.
Yesu Awatahadharisha Watu Kuhusu Walimu Wa Shera
38 Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi yao rasmi na kusalimiwa kwa heshima masokoni. 39 Pia wao hupenda kukaa viti vya mbele katika masinagogi na kupewa nafasi za heshi ma katika sherehe. 40 Hao hao ndio huwadhulumu wajane nyumba zao na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Mungu ata waadhibu vikali zaidi.”
Sadaka Ya Mjane
41 Kisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha. 42 Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.
43 Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninawaambia hakika, huyu mjane ametoa zaidi kuliko wote! 44 Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao; lakini huyu mama ingawa ni fukara, ameweka kila kitu alichokuwa nacho, hata na kile alicho hitaji kwa ajili ya riziki yake.”

Copyright © 1989 by Biblica