Marko 10:13-31
Neno: Bibilia Takatifu
Yesu Anawabariki Watoto Wadogo
13 Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse lakini wanafunzi wake wakawakemea. 14 Yesu alipoona yaliyokuwa yakitokea alichukizwa, akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa watu kama hawa! 15 Ninawahakikishieni kwamba, mtu ye yote ambaye hataukubali Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.” 16 Akawakumbatia wale watoto wadogo, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.
Mtu Tajiri
17 Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake akamwuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini niurithi Ufalme wa milele?”
18 Yesu akamwambia, “Mbona unaniita mwema? Hakuna ali yemwema isipokuwa Mungu peke yake. 19 Unazifahamu amri ‘Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye. Waheshimu baba yako na mama yako .”’
20 Akamjibu, “Mwalimu, amri hizi zote nimezishika tangu nikiwa mtoto.”
21 Yesu akamtazama kwa moyo wa upendo akamwambia, “Umepun gukiwa na kitu kimoja tu. Nenda ukauze vitu vyote ulivyo navyo uwape maskini fedha utakazopata, nawe utakuwa na utajiri mbin guni; kisha njoo, unifuate.”
22 Yule mtu aliposikia hayo, alisikitika sana, akaondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa tajiri sana.
23 Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa
Mungu!”
24 Wanafunzi wake wakashtushwa sana na maneno hayo. Lakini Yesu akasema tena, “Wanangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalme wa Mungu. 25 Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”
26 Wanafunzi wake wakashangaa mno. Wakaulizana wao kwa wao, “Ni nani basi anaweza kuokolewa?”
27 Yesu akawatazama akawaambia, “Kwa wanadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu.” 28 Petro akaanza kumwambia, “Sisi tumeacha kila kitu tukakufu ata!”
29 Yesu akajibu, “Ninawaambieni hakika, hakuna mtu ye yote aliyeacha nyumba, kaka, dada, mama, baba, watoto au shamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya kuitangaza Habari Njema, 30 ambaye hatalipwa katika ulimwengu huu mara mia zaidi: nyumba, kaka, dada, mama, watoto, mashamba na mateso pia; na kupewa uzima wa milele katika ulimwengu ujao. 31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na wa mwisho watakuwa wa kwanza.”
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica