Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji

Huu ni mwanzo wa Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Kama alivyoandika nabii Isaya, Mungu alisema: “Namtuma mjumbe wangu akutangulie, ambaye ataandaa njia yako.” “Mtu aitaye kwa sauti kuu jangwani. ‘Mtengenezeeni Bwana njia; nyoosheni sehemu zote atakazopitia.’ ”

Yohana alitokea nyikani, akawabatiza watu huko na kuwahubi ria kwamba watubu, wabatizwe, ili wasamehewe dhambi zao. Watu kutoka eneo lote la Yudea na sehemu zote za Yerusalemu walikwenda kumsikiliza. Wakatubu dhambi zao, akawabatiza katika mto wa Yor dani. Yohana alivaa mavazi ya manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa ni nzige na asali ya mwituni. Naye alihubiri akisema, “Baada yangu anakuja mwenye uwezo kunizidi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawaba tiza kwa Roho Mtakatifu.”

Yesu Abatizwa

Baadaye Yesu akaja kutoka Nazareti katika sehemu ya Gali laya, akabatizwa na Yohana katika mto wa Yordani. 10 Yesu alipo toka kwenye maji aliona mbingu zikifunuka na Roho wa Mungu anam shukia kama njiwa. 11 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni mwanangu mpendwa; nimependezwa nawe.”

Yesu Ajaribiwa Nyikani

12 Mara tu baada ya haya, Roho akamwongoza Yesu mpaka nyikani. 13 Akakaa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini aki jaribiwa na shetani. Alikaa na wanyama wa porini na malaika wal imhudumia.

Yesu Aanza Kuhubiri

14 Yohana mbatizaji alipokamatwa na kutiwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya akaanza kutangaza Habari Njema za Mungu, 15 akisema, “Wakati umefika: Ufalme wa Mungu umewasili. Tubuni, muamini Habari Njema.”

Yesu Awaita Wanafunzi Wanne

16 Yesu alipokuwa akitembea kando kando ya Ziwa la Galilaya alimwona Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa kutumia nyavu; ndugu hawa wawili walikuwa wavuvi. 17 Yesu akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” 18 Wakaacha nyavu zao mara moja wakamfuata Yesu.

19 Alipokwenda mbele kidogo, akawaona Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo. Wao walikuwa katika mashua wakitengeneza nyavu zao. 20 Mara tu alipowaona akawaita, nao wakamwacha baba yao na wavuvi wa kuajiriwa, wakamfuata Yesu.

Yesu Afukuza Pepo Mchafu

21 Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya sabato, Yesu akaenda katika sinagogi akaanza kufundisha. 22 Watu waliom sikiliza, walishangazwa sana na mafundisho yake. Yeye hakufund isha kama walimu wao wa sheria. Alifundisha kama mtu mwenye mam laka.

23 Wakati huo huo, mtu mmoja aliyekuwa na pepo 24 akapiga kelele humo katika sinagogi akasema, “Mbona unatuingilia, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Ninafahamu wewe ni nani! Wewe ni Mtakatifu wa Mungu.” 25 Lakini Yesu akamkemea akamwambia, “Kaa kimya! Mtoke!” 26 Yule pepo mchafu akamtikisa yule mtu kwa nguvu kisha akamtoka akipiga kelele.

27 Watu wakashangaa, wakaanza kuulizana, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya? Huyu mtu anatoa amri kwa mamlaka na hata pepo wanamtii!”

28 Sifa zake zikaenea upesi kila mahali katika mkoa wote wa

Yesu Amponya Mama Mkwe Wa Simoni

29 Yesu na wanafunzi wake walipoondoka katika sinagogi, walikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea. Wanafunzi wengine waliokuwepo ni Yakobo na Yohana. 30 Mama mkwe wake Simoni alikuwa kitandani, ana homa. Na mara Yesu alipofika wakamweleza. 31 Yesu akaenda karibu na kitanda, akamshika yule mama mkono, akamwinua; homa ikamtoka, akawahudumia.

Yesu Aponya Wengi

32 Jioni ile, baada ya jua kutua, watu wakawaleta wagonjwa wote na wengine waliopagawa na pepo kwa Yesu. 33 Watu wote wa mji huo wakakusanyika mbele ya nyumba hiyo. 34 Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya kila aina. Akawatoa pepo wengi; lakini hakuwaruhusu pepo hao wazungumze, kwa sababu wal ifahamu yeye ni nani.

Yesu Aondoka Kapernaumu Na Kwenda Galilaya

35 Kesho yake alfajiri, kabla hapajapambazuka, Yesu akaamka akaenda mahali pa faragha, akaomba. 36 Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta. 37 Walipomwona wakamwambia, “Kila mtu ana kutafuta!”

38 Yesu akawajibu, “Twendeni kwenye vijiji vingine vya jirani nikahubiri huko pia; kwa sababu hicho ndicho kilicho nileta.” 39 Kwa hiyo akazunguka Galilaya nzima akihubiri katika masinagogi na kuponya watu waliopagawa na pepo.

Yesu Amponya Mtu Mwenye Ukoma

40 Akaja mtu mwenye ukoma, akapiga magoti mbele ya Yesu akamsihi, “Ukitaka, unaweza kunitakasa.” 41 Yesu akamwonea huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka upone, takasika.” 42 Mara ukoma wote ukaisha akapona kabisa. 43 Yesu akamruhusu aende lakini 44 akamwonya, “Usimwambie mtu ye yote habari hizi; bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka ya utakaso kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwa watu.”

45 Lakini yule mtu alikwenda akatangaza habari za kuponywa kwake kila mahali. Kwa hiyo Yesu hakuweza tena kuingia katika vijiji na miji waziwazi isipokuwa alikaa sehemu zisizo na watu, nao wakamfuata huko kutoka pande zote.