Add parallel Print Page Options

32 Ilipofika jioni, baada ya jua kuzama waliwaleta kwake watu wote waliokuwa wagonjwa na waliokaliwa na mashetani. 33 Mji mzima ulikusanyika mlangoni pale. 34 Naye akawaponya watu waliokuwa na magonjwa ya kila aina, na kufukuza mashetani wengi. Lakini yeye hakuyaruhusu mashetani kusema, kwa sababu yalimjua.[a]

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:34 mashetani … yalimjua Mashetani yalifahamu kuwa Yesu alikuwa ni Masihi, mwana wa Mungu. Tazama Mk 3:11-12.